DKT. GWAJIMA AZINDUA BARAZA LA WAZEE LA TAIFA ,ASEMA MATAMANIO YA WAZEE WOTE NCHINI SASA YAMEFIKIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 11, 2022

DKT. GWAJIMA AZINDUA BARAZA LA WAZEE LA TAIFA ,ASEMA MATAMANIO YA WAZEE WOTE NCHINI SASA YAMEFIKIWA


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima



Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima na Mwenyekiti wa mtandao wa mashirika yasiyo ya Kiserikali Bi.Clotilda Kokupima wakiserebuka kwa furaha baada ya uzinduzi wa Baraza la Wazee la Taifa mapema hii leo jijini Dodoma

Mwenyekiti wa mtandao wa mashirika yasiyo ya Kiserikali Bi.Clotilda Kokupima akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum



Na,Okuly Julius, Dodoma 
Uwepo wa Baraza la Taifa la Wazee imekuwa ni matamanio ya Wazee wote nchini, hususani baada ya kumaliza zoezi la uundaji wa Mabaraza hayo ngazi za Mikoa, Halmashauri, Kata na vijiji/Mitaa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima wakati akizindua Baraza la Taifa la Wazee mapema hii leo March,11,2022 jijini Dodoma.

Dkt.Gwajima amesema kuwa anakumbuka tangu akiwa Naibu Katibu Mkuu OR - TAMISEMI, pia akiwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum amekuwa akipokea maoni na maswali mengi kutoka kwa wadau na Wazee wenyewe kuhusu lini Baraza hili litaundwa na kuzinduliwa.

Ambapo amebainisha kuwa maswali haya yote yalikuwa na nia njema kabisa katika kuweka misingi ya upatikanaji wa chombo hicho muhimu kwa haki na Ustawi wa Wazee nchini na kwa furaha kubwa ndoto hiyo imetimia hii leo baada ya kuzindua Baraza hilo.

Dkt.Gwajima ametambua na kukumbusha vizuri historia ya nchi yetu hasa mchango mkubwa uliotolewa na Wazee kabla na baada ya Uhuru na akikumbusha kwamba katika kudai Uhuru, mafanikio ya Hayati Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere yalitokana na baraka za Wazee kwa kumuombea kwa Mwenyezi Mungu akamilishe azma ya kuiongoza nchi yetu kujitawala yenyewe.

Hata baada ya Uhuru, Mwalimu Nyerere aliendelea kutumia jumuia za wazee kuelezea masuala mazito ya nchi yetu.

Aidha viongozi wa Awamu zote za serikali zilizofuata waliendeleza utamaduni huo wa kuwatumia wazee wakati wote walipokuwa na jambo zito la kulieleza kwa wananchi.

Ikumbukwe pia, mwezi Mei, 2022 Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliongea na Taifa kupitia jijini Dar es Salaam na kuahidi maboresho makubwa katika huduma za kijamii kwa wazee.

Hivyo inamaanisha kuwa jamii inatakiwa kuendelea kutambua msingi imara wa nchi uliojengwa na wazee katika maendeleo ya nchi yetu.

Sura ya 3, Ibara ya 3.14 ya Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003, imeelekeza kuundwa kwa Mabaraza ya Ushauri ya Wazee katika ngazi za Vijiji/Mitaa, Wilaya, Mkoa na Taifa ambayo pamoja na majukumu mengine yatasaidia katika kuhamasisha familia na jamii kutekeleza wajibu wao wa kuwatunza wazee wao, hivyo serikali imekuwa ikifanya jitihada za kusimamia uundaji wa Mabaraza ya Wazee katika ngazi zote, kuanzia Vijiji/Mitaa, Kata, Halmashauri na Mikoa.

"Jumla ya mabaraza 47,876 yamekwisha anzishwa. Nawapongeza sana Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Maafisa Ustawi wa Jamii wote nchini kusimamia mchakato huu. Nawaomba waendelee kuyalea mabaraza hayo na kuhakikisha kwamba yanatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sera na miongoz iliyopo" Amesema Dkt Gwajima

Aidha serikali imeendelea kuwajali wazee kwa kuweka utaratibu na mifumo ya afua kwa wazee kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamia upatikanaji wa huduma za matibabu kwa kuwapatia vitambulisho vya kuwawezesha kupata matibabu bila malipo. Hadi kufikia sasa jumla ya wazee 1,256,544 wamepatiwa vitambulisho hivyo,Kuanzisha madirisha 2,335 ya kutolea huduma za afya kwa wazee katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini,Kudhibiti mauaji ya wazee kwa kutekeleza Mkakati wa Kutokomeza mauaji ya Wazee. Katika kutekeleza mkakati huu mauaji ya wazee yamepungua kutoka wazee 190(ME 88 NA KE 102) kwa mwaka 2015 na hadi kufikia 54(ME 20 NA KE 32) mwaka 2020.

Pamoja na hayo Serikali imeboresha makazi ya wazee kwa kukarabati na kujenga miundombinu mipya katika makazi ya wazee ya Kolandoto (Shinyanga), Nunge (Dares Salaam), Njoro (Kilimanjaro), Magugu (Manyara) na Fungafunga(Morogoro),Kutoa huduma ya matunzo kwa wazee kwenye Makazi 14 yanayo endeshwa na serikali yenye jumla ya wazee 277(ME 166 NA KE 111).
Jumla ya wazee 292,844 wamepatiwa huduma za matibabu katika hospitali za mikoa,kanda na taifa kuanzia juni 2021 hadi januari 2022

"Licha ya nia nzuri ya serikali, natambua bado zipo changamoto katika utoaji wa huduma kwa wazee katika maeneo mbalimbali. Hivyo nawaomba wajumbe wa Baraza hili la Taifa kuchakata vizuri maoni ya namna gani tunaweza kuboresha zaidi upatikanaji wa haki na ustawi wa wazee katika nchi yetu"Amesema

"Naahidi kwamba maoni hayo tutayafanyika kazi. Wizara yangu kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii inalo jukumu la Kisheria la kuhakikisha kwamba huduma za kijamii kwa makundi maalum zinatolewa kwa viwango stahili, na sisi viongozi wa Wizara tutaendelea kusimamia hilo" Ameongeza

Kuhusu swala la sera na sheria Dkt Gwajima amesema kuwa Wizara bado ipo katika hatua za kuhuisha Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 na kuanza mchakato wa utungaji wa Sheria ya Wazee.

Kwa upande wake Mwanyekiti Mteule wa Baraza la Wazee la Taifa Lameck Sendo amekaizia juu ya uundwaji wa sheria za wazee kwa sababu hakuna haja ya kuwa na sera nyingi bila sheria hivyo akamuomba Waziri Mheshimiwa Dkt Dorothy Gwajima kuwasaidia kufikisha maombi yao kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuundiwa sheria zao badala ya kuendelea kubaki na sera.

Nae Mwenyekiti wa mtandao wa mashirika yasiyo ya Kiserikali Bi.Clotilda Kokupima ameishukuru serikali kwa kukamilisha uzinduzi wa Baraza hili la taifa la wazee akibinisha kuwa sasa wazee wamepata chombo mahususi ya kufikisha changamoto zao na kupatiwa ufumbuzi. 

No comments:

Post a Comment