KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma yaridhishwa na mradi wa ujenzi wa soko la wazi la Machinga - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 22, 2022

KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma yaridhishwa na mradi wa ujenzi wa soko la wazi la Machinga


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Godwini Mkanwa

Na Okuly Julius Dodoma 

KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma imetembelea mradi wa ujenzi wa soko la wazi la Machinga ili kujionea hali halisi ambapo imeridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa soko hilo ambao umefikia asilimia 67 huku ikiutaka uongozi wa Jiji la Dodoma kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

Akiongoza Kamati hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Godwini Mkanwa leo jijini Dodoma mara baada ya ziara fupi ya kamati hiyo amesema kuwa soko hilo hatua iliyofikia inardhisha hivyo Wamachinga wakae mkao wa kufanya biashara zao katika mazingira salama na kuvutia.

“Hakika sisi kama Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma tumeridhishwa na ujenzi wa soko hili kwani unaendelea vizuri jambo la muhimu sasa ni wajibu wa Halmashauri ya jiji la Dodoma kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati ili wamachina wahamie hapa waendelee kufanya biashara zao kwa amani,”alisema

Pia ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka wamachinga kuweza kukua kiuchumi na Taifa kwa ujumla.

Mkanwa ameagiza Halmashauri ya jiji la Dodoma kuzingatia viwango sahihi vya kodi ili kuepuka dosari ambazo zinaweza kujitokeza.

"Sanjari nataka muweke viwango rafiki kwa wamchinga msije mkaweka viwango ambavyo Rais, au Waziri Mkuu akija naye anashusha viwango mtakuwa mmedharirishwa hivyo ni bora mkaweka viwango rafiki ambayo havitaegemea upande wowote na katika hili ni vyema mkashirikisha wamachinga wenyewe,”alibainisha

kwa upande wake katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga amesema ujenzi wa soko hilo la kisasa utasaidia kupendezesha jiji na kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato.

Pili ameipongeza serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia kwa kugusa kundi kubwa la wamachinga ambao wamejiajiri katika maeneo mbalimbali.

“Tumepata taarifa kuwa soko hili litakuwa na uwezo wa kuchukua wamachinga 2,938 ni watu wengi hivyo unategemea kuona baada ya kukamilika kwa soko hili jiji letulitakuwa safi na ongezeko la watu wanaolipa kodi,”alisema

Naye Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Francis Kaunda amesema kujengwa kwa mradi huo kutakuwa na faida nyingi kwa jiji la Dodoma, wafanyabiashara na taifa kwa ujumla.

Amezitaja faida hizo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapato ambapo kukamilika kwa mradi huo jiji la Dodoma linatarajia kukusanya sh.bilion 1.1 kwa mwaka kutokana na kodi mbalimbali zitakazotozwa kwa baadhi ya huduma katika eneo hilo ikiwemo maegesho ya magari,vyoo, na mbao za matangazo.

Amsema faida nyingine ni kuliweka jiji la Dodoma katika hali ya usafina kurahisisha shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira

“Kuwahakikishia usalama wafanyabiashara ndogo ndogo katika jiji la Dodoma kwa kuwa katika eneo maalumu ambapo wafanyabiashara wapatao 2,938 watakuwa na ajira za uhakika kwa kufanya biashara zao katika eneo maalumu linalotambulika,”alisema

Kaunda amemalizia kwa kusema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili ambao utagharimu sh.bilioni 7.5.




No comments:

Post a Comment