![]() |
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana Ajira na wenye ulemavu Prof Joyce Ndalichako akizungumza katika uzinduzi wa Baraza jipya la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu. |
![]() |
Prof Jamal Katundu Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana Ajira na wenye ulemavu akizungumza katika uzinduzi wa baraza jipya la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo jijini Dodoma. |
![]() |
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana Ajira na wenye ulemavu na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Patrobas Katambi (wa pili Kushoto) kwenye picha ya pamoja |
Na Okuly Julius Dodoma
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana Ajira na wenye ulemavu Prof Joyce Ndalichako amewasisitiza baraza la wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu kufuata taratibu na miongozo ya kazi pamoja na kuwa na mshikamano.
Akizindua Baraza la Bafanyakazi leo jijini Dodoma Waziri Ndalichako amesema kuwa mshikamoja wa pamoja ni sehemu ya mafanikio ya kazi za kila siku wanazozifanya hivyo kila mmoja analojukumu la kuzingatia muda wa kazi ndiyo nguzo ya mafanikio.
Pia ameongeza kuwa tamaa yake kama Waziri ni kuona watumishi wa Ofisi ya Waziri mkuu wanashika nambari moja katika utekelezaji wa majukumu yao na endapo ikitokea kupanga Wizara kwa namba basi washike namba moja kiutendaji na wawe mfano wa kuigwa.
"Nataka kuona utendaji bora kwa kila mmoja wetu tukizingatia kanuni na sheria za utumishi wa Umma hiyo ndio itakuwa njia ya kuelekea kutimiza malengo ya serikali hii ya Awamu ya sita," Amesema
Aidha, Prof Ndalichako amesema kuwa wizara yake haitomvumilia mtumishi yoyote atakayejihusisha na vitendo vya Rushwa katika kutoa huduma.
Amesema kuwa Wizara yake inafanya kazi kubwa sana ya kwenda kukagua watu katika ofisi zao wenye ushawishi mkubwa na inawezekana hawajafuata sheria katika kuajiri na kwenye kazi zao kwa ujumla hivyo anaweza kutumia mwanya huo kumrubuni mkaguzi ili kumpa hata safi ya kazi yake ila hiyo ni kinyume na sheria.
Sitavumilia mtumishi yeyote atakayejaribu kucheza na ofisi yangu hapo ndipo mtaona rangi zangu zote usijaribu kucheza na pesa zozote zinazotolewa kwa ajili ya kazi narudia tena usijaribu," Ameongeza
Prof Ndalichako amewasihi watumishi wote kuwa wabunifu na wasifanye kazi kwa mazoea ili kuongeza tija katika sehemu ya kazi wanayofanya.
No comments:
Post a Comment