Kuelekea kilele cha siku ya wanawake Duniani ambapo hufanyika kila ifikapo March 8 kila mwaka,Askari wa kike wa vyombo vya ulinzi na usalama wameandaa Kongamano litalofanyika Wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Katika Maadhimisho ya Mwaka huu imebebwa kauli mbiu isemayo ''Tuimarishe usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake vijijini ''
Katika Kongomano hilo Mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maluum Mh,Mwanaidi Ali Khamis.
KONGAMANO LA WANAWAKE WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI LIMEANZA KUFANYIKA LEO KATIKA UKUMBI WA BUNGE WA PIUS MSEKWA NA TAREHE 08 MARCH WAPIGANAJI WATAUNGANA NA WENZAO KWENDA CHEMBA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
Okulyblog.blogspot.com inawatakia maandalizi mema wanawake wote duniani kuelekea siku hii muhimu kwao.


No comments:
Post a Comment