![]() |
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe |
Dar es salaam
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Zuhura Yunus imesema kuwa Mwenyekiti huyo amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kujali kwake huku akikubali kwa msingi mkubwa wa kujenga Taifa la Tanzania ni kusimamia haki.
Pia Mbowe ameeleza kwamba wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na za kiungwana na kwamba yupo tayari kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo ili nao waweze kutekeleza majulumu yao ipasavyo.
" Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki," ilisema taarifa hiyo.
Mbowe na wenzake watatu wameachiliwa huru baada ya mwendesha Mashtaka mkuu wa serikali kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi katika Mahakama ya Divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.
Mahakama hiyo ilikuwa ikiwashikilia kwa kesi ya kujibu kuhusu tuhuma mbalimbali zikiwamo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi.
Kesi hiyo ilikuwa ikisimamiwa na jaji Joachim Tiganga.
No comments:
Post a Comment