![]() |
| Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu[Kazi ajira,vijana ,na wenye ulemavu]Prof.Joyce Ndalichako (kushoto) na Rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania[TUCTA] Tumaini Nyamhokya (kulia) |
![]() |
| Baadhi ya Washiriki waliohudhurua ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania[TUCTA] |
Na.Okuly Julius, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu[Kazi ajira,vijana ,na wenye ulemavu]Prof.Joyce Ndalichako amepiga marufuku kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini juu ya tabia ya kuwaweka ndani[kortini] watumishi wa umma wenye makosa yasiyo ya jinai.
Marufuku hiyo ameipiga hii leo Machi 12,2022 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania[TUCTA] ambapo amesema haipaswi kuwekwa ndani watumishi wa umma kwa makossa yasiyo ya jinai kwani pamekuwa na tabia ya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuwaweka ndani watumishi wa umma kwa makosa yasiyo ya jinai.
Hivyo,amesema makosa ya kiutendaji kwa watumishi yachukuliwe hatua sehemu za kazi kwa sababu serikali ilishatoa maelekezo ambapo sheria hizo zimetoa mwanya kwa Waajiri kuwachukulia hatua watumishi ambo ni Wazembe kazini ,Utovu wa nidhamu na wale watumishi ambao hawawajibiki ipasvyo sehemu za kazi.
Ambapo, ameongeza kuwa Waajiri watumie Sheria za mahusiano makazini na ile sheria za utumishi wa umma katika kuwachulia hatua watumishi wenye utovu wa nidhamu na maadili mabaya na akawataka Watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia sheria za kazi zilizopo.
Aidha,Prof.Ndalichako amewaagiza waajiri wote nchini kuhakikisha vikao vya mabaraza ya wafanyakazi vifanyike kwa mujibu wa matakwa ya kisheria ikiwemo kulipa posho stahiki kwa wafanyakazi.
Pia waajiri wahakikishe kuwa mabaraza yanapopita muda wake wafanye haraka kuyahuisha ili kuendelea kutimiza takwa la kisheria ikiwemo kulinda maslahi ya wafanyakazi,kumshauri muajiri juu ya maswala mbalimbali yahusuyo ufanisi wa kazi na maendeleo ya wafanyakazi kwa ujumla.
KWA UPANDE wake Rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania[TUCTA] Tumaini Nyamhokya amesema kuna haja kwa serikali kutekeleza ipasavyo kuwarejesha kazini watumishi wa darasa la saba kwani kuna baadhi ya taasisi zimekuwa zikiwakataa na kuwanyima stahiki zao .
NAYE Mwenyekiti wa Kamati ya wanawake wa Shirikisho hilo Rehema Ludanga akibainisha kuwa bado kuna changamoto ya utekelezaji wa sheria ya mkataba wa kazi ambapo mwajiriwa anapaswa kupatiwa mkataba wa Miezi kumi na mbili ila mpaka sasa kuna waajiri ambao wanaendelea kutoa mikataba iliyo chini ya miezi kumi na mbili jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Tazama video hapo Chini






No comments:
Post a Comment