Na Okuly Julius Dodoma
Akizungumza March 23,2022 mara baada ya kufanya ziara ya kutathmini na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya halmashauri ya jiji la Dodoma Katibu Mkuu wa ALAT taifa Elirehema Moses Kaaya amesema kuwa ubunifu mkubwa wa miradi unaofanywa na wafanyakazi wa Jiji la Dodoma ndio matokeo chanya ya utekelezaji wa miradi hii hasa kwa kuzingatia kwa sehemu kubwa wanatumia mapato ya ndani.
Pia ameridhishwa kwa kiwango kikubwa na Maendeleo ya ujenzi wa Soko la wazi la Machinga pamoja na Madarasa ya UVIKO -19 yaliyojengwa katika Shule ya Umonga na kusema kuwa madarasa hayo yameonyesha thamani ya pesa kwa sababu yamejengwa katika kiwango kizuri.
"Miradi yote niliyotembelea leo ndani ya Halmashauri ya jiji la Dodoma kiukweli imenionesha thamani ya pesa kwa sababu imetekelezwa katika viwango vikubwa sana nkwa kuzingatia ubora na ufanisi nimependa sana ubunifi wenu hasa katika ujenzi wa Soko la wazi la Wamachinga,"Amesema Elirehema Moses Kaaya.
Ameipongeza pia Halmashauri ya jiji la Dodoma kwa kubuni na kujenga vitega uchumi vyake kwa kutumia fedha zake za ndani ikiwemo MTUMBA INVESTMENT NA DODOMA CITY HOTEL huku akiamini kuwa mara baada ya miradi hiyo kukamilika na kuanza kufanya kazi itakuwa ni sehemu tosha kabisa kwa Halmashauri kujipatia mapato ya kutosha kutekeleza miradi mingine ya maendeleo kwa wananchi wake.
Aidha,Elirehema ameongeza kuwa mafanikio yote haya ni kutokana na kuwa na uongozi madhubuti na wenye maono na malengo ya kuifikisha Tanzania katika viwango vya juu kiuchumi chini ya Rais wa Awamu ya Sita Mh.Samia Suluhu Hassan na kuongeza kuwa Rais anastahili sifa kutokana na kazi inayoonekana hivyo ni vyema tukazisema kwa wananchi ili kila mmoja ajue mazuri yanayotekelezwa na serikali yake.
"Mazuri yanapotendaka tuseme na sisi kama ALAT tunaapa kuyaahubiri iwe jua au mvua mazuri yato yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ni lazima tuyaseme kwa wananchi wayajue kiukweli Mama anaupiga mwingi sana," Amesema Elirehema Moses Kaaya
Kwa Upande wake Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Francis Kaunda wakati akiwasilisha taarifa ya miradi hiyo amesema kuwa Jiji la Dodoma katika kutekeleza miradi yake
Imekuwa kutumia fedha za ndani na maamuzi haya yamepitishwa kwa kushirikiana na madiwani wote.
Ambapo amesema kuwa jiji lilipokea fedha mbalimbali kutoka Serikali kuu na zimetumika katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa 143 vya sekondari, 4 vya msingi,Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Hombolo Makulu ambapo mpaka sasa ujenzi huo unaendelea,Kituo cha Afya Chang'ombe na Fedha zingine milioni 500 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
Ameongeza kuwa katika miradi ya kimkakati ikiwemo Soko la wazi la Machinga ,Mtumba Investment na Dodoma City Hotel jiji inatumia mapato yake ya ndani kukamilisha miradi hiyo ambapo gharama za Ujenzi wa Soko la wazi ni Bilion 7.5,Dodoma city Hotel ni bilioni 9.9 wakati ule mradi wa Mtumba Investment wenyewe utagharimu kiasi cha Bilioni 59 na fedha zote hizo zinatokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya jiji la Dodoma.
Pia Kaunda amemalizia kwa kusema kuwa nia ya Halmashauri ya jijini la Dodoma ni kujitegemea yenyewe kimapato na katika kutekeleza miradi yake ya kimkakata ili kutengeneza vyanzo vingi vya mapato jambo ambalo litawajengea uwezo wa kujitegemea.
"Nia na Malengo yetu kama jiji ni kusimama wenyewe na kujitegemea na ndio maana tunapambana sana katika kubuni vyanzo vipya vya mapato,"Amemalia Kaunda
No comments:
Post a Comment