| Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa na |
Kutokana na ugonjwa wa homa ya manjano kuripotiwa nchini Kenya Machi,3,2022 katika Kaunti ya Isiolo kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shirika la Afya Duniani [WHO]. Wizara ya Afya imetoa tahadhari kwa wananchi kujikinga na ugonjwa huo.
Hayo yamesemwa leo Machi 9,2022 na waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma amesema kuna tetesi zingine kutokea nchini Uganda hivyo wizara ya Afya imejipanga kudhibiti ugonjwa huo ambapo baada ya uchunguzi wa wizara bado ugonjwa haujaingia nchini .
Waziri Ummy ameanisha miongoni mwa dalili za ugonjwa wa homa ya manjano kuwa ni pamoja na kutokwa damu puani,kuumwa na kichwa.
AidhaWaziri Ummy ametaja nchi barani Afrika zilizo hatari kukumbwa na wimbi la ugonjwa wa homa ya manjano kuwa ni pamoja na Angola, Benin ,Burkina faso ,Burundi,Cameroon,Jamhuri ya Afrika ya kati,Chad,Ivory Coast DRC Congo ,Guine Ikweta ,Gabon,Gambia,Guine,Guine Bissau,Kenya ,Liberia .Mali,Mauritania,Niger,Nigeria,Rwanda,Senegal,Sierra Leone ,Sudan Kusini,Togo,na Uganda.
Hata hivyo,ameanisha mikakati ya Wizara katika mapambano ya ugonjwa huo ni pamoja na kuchanja kwa wasafiri ambapo kwa nchi za Afrika mashariki gharama za chanjo ni Tsh.30,00 huku akiagiza wataalam wa afya kwenda mipakani katika kuhakikisha mtu anayeingia nchini kutoka nchi zenye idadi kubwa ya watu wenye ugonjwa huo wanachanjwa homa ya manjano.
Mwakilishi Mkaaziwa shirika la Afya Duniani [WHO] Dkt.Tigest Katsela Mgestu amesema asilimia 60 ya wagonjwa wa homa ya manjano hufariki unia huku akibainisha sababu za kuitwa homa ya manjano ni kutokana mwili pamoja na macho kuwa na rangi ya njano.
Ikumbukwe kuwa ,katika nchi za Afrika Mashariki, Tanzania haijawahi kuwa na taarifa ya mgonjwa yeyote aliyethibitika kuwa na ugonjwa wa Homa ya Manjano tangu mwaka 1950



No comments:
Post a Comment