![]() |
| Baadhi ya Washiriki katika Hafla ya Uzinduzi ya Bodi ya Wakurugenzi wa wataalamu wa ununuzi na ugavi |
![]() |
| Baadhi ya Washiriki katika Hafla ya Uzinduzi ya Bodi ya Wakurugenzi wa wataalamu wa ununuzi na ugavi |
Na.Okuly Julius, Dodoma
Hayo yamesemwa jijini Dodoma hii leo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Lawrence Mafuru kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Mwigulu Nchemba katika halfa fupi ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya bodi ya wataalam wa ununuzi na ugavi(PSPTB),ambapo ametoa wito kwa bodi hiyo kwenda kusimamia kwa ukamilifua Sheria waliyoianzisha wenyewe.
"Naomba mtambue kuwa wadau wa ununuzi na ugavi wana matumaini makubwa kutoka kwenu kwani nyie ndio mtatoa dira ya chanya katika kutekeleza majuku yao na hii inajumuisha usimamizi wa maadili na mienendo ya Wataalam, uhuwishwaji na utengenezaji wa mitaala unaozingatia umahiri wa kitaaluma na mahitaji ya soko"Amesema Mafuru
Aidha amewahakikishia kuwa serikali kupitia Wizara hiyo itawapa ushirikiano kwa hatua zinazolenga kuondoa kabisa uzembe na ukiukwaji wa maadili katika fani ya ununuzi na ugavi kwani pesa nyingi za serikali, zinatumika kupitia taaluma hiyo.
Pia niwaombe kuhakikisha waajiri wote wanatoa ushirikiano kwa Bodi hii, haswa linapokuja suala la usimamizi wa maadili kwa wataalam waliosajiliwa na Bodi.
Ameongeza kuwa Waajiri wanapaswa kutoa taarifa kwenye Bodi zinazohusiana na ukiukwaji wa maadili kwa wataalam, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwani hakuna ufanisi bila maadili na weledi na mhakikishe waajiri wote wanaajiri watumishi wenye sifa stahiki zinazotambuliwa na sheria ya PSPTB na kuzingatia mahitaji yaliyopo kwenye Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Na. 3 wa mwaka 2015 wa kada zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.
"Wizara yangu itaendelea kuisaidia Bodi ili iweze kutekeleza majukumu yake kama ulivyoanisha kwenye hotuba yako napenda kusisitiza usimamizi mzuri wa rasilimali watu pamoja na matumizi sahihi ya rasilimali fedha ili malengo yaliyopangwa na PSPTB yaweze kutekelezwa kwa ufanisi,"ameongeza.
KWA UPANDE wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PSPTB,Jacob Kibona ameeleza kuwa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi, imepewa jukumu la kusimamia misingi ya taaluma ya ununuzi na ugavi na mienendo ya wataalamu wake.
Pia amesema Bodi inawajibu wa kuzalisha wataalam wenye weledi na uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili na miiko ya taaluma yao hivyo ameahidi kuwa Bodi yake itasimamia na kuimarisha taaluma ya ununuzi na ugavi sambamba na kuongeza nguvu ya kupambana na vitendo vyote vinavyokinzana na maadili ya kitaaluma ya ununuzi na ugavi kama ubadhirifu wa mali, rushwa na ukiukwaji wa taratibu za ununuzi na ugavi.
"Hili litakuwa ni kipaumbele kwa Bodi yangu ili tuweze kuwa na wataalam waadilifu wanaosimamia zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya Serikali inayoelekezwa kwenye manunuzi,"amesema Kibona.
Pamoja na hayo ameeleza mambo yanayolengwa kutekelezwa na PSPTB ni kukamilisha kufanya utafiti wa kitaalamu ambao umesimama kwa sababu ya kukosa fedha, uendeshaji wa taratibu za maadili ya wataalamu wa ununuzi na ugavi,utengenezaji wa mitaala ya kitaaluma, kuandaa agenda za utafiti (Research Agenda) ambazo zitatumiwa na Wataalam kufanya tafiti za kisayansi na kuishauri Serikali juu ya uboreshaji wa Taaluma ya Ununuzi na Ugavi na kutengeneza viwango vya ubora katika taaluma na kujenga ofisi Makao makuu Dodoma katika kiwanja kilichopo eneo la Medeli ambapo michoro imeshawasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango.







No comments:
Post a Comment