| Waziri mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wananchi baada ya kukamilika ukaguzi wa Jengo la wazi la Wamachinga jijini Dodoma eneo la Bahiroad |
Na.Okuly Julius, Dodoma
Jengo hilo litakalokuwa na wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga zaidi 3000 linajengwa kwa fedha za ndani za Jiji la Dodoma na serikali kuu ambapo hadi kukamilika kwake itagharimu takriban bilioni 7.5.
Katika ukaguzi huo Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameridhishwa na kuvutiwa na muonekano wa Jengo hilo katika ramani na kusema kuwa mradi huo ndio namba moja kwa sasa hapa nchini.
Amewataka wakuu wengine wa Mikao kuiga mfano huu wa Jiji la Dodoma wa kujenge masoko kwa ajili ya Wamachinga kulingana na mazingira huku akitoa rai kwa viongozi mbalimbali wa mikoa kuwashirikisha vyema wafanyabishara ndogondogo katika vikao ili kuchagua maeneo ambayo wanatamani kujengewa majengo ya wazi kwa ajili ya biashara.
Kwa upande wake Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa ameupongeza ubunifu uliofanywa na jiji la Dodoma huku akiongeza kuwa mradi huu utakuwa wa mfano na atawaagiza wakuu wengine wa mikoa kutembelea mradi huo ili kujionea jinsi Jengo hilo linavyojengwa ili nao wakajenge katika mazingira yao.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema kuwa jengo hilo litakapokamilika hakuna Machinga atakayebakia mjini wote watatakiwa kuwepo katika soko hilo.
Wakati Huo huo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri yeye amaewataka majirani wanaolizinguka jengo hilo kuhakikisha wanapaka rangi nyekundu mabati yao ili kupendezesha mandhari ya soko hilo.
Awali Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema kuwa Jengo hilo Jipya la wazi la Machinga Complex litakamilika rasmi May mwaka huu badala ya March 17 kama ilivyotangazwa hapo mwanzo huku akiwataka Wachinga kuendelea kujiandikisha kwa ajili ya utaratabu wa kupata vibanda pindi soko hilo litakapo kamilika.
Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe ameelezea jinsi Baraza la madiwani lilivyokubaliana na jiji kwa kutoa sehemu ya fedha za ujenzi wa soko hilo muhimu kwa wamachinga na uchumi wa jiji hilo.
Akimalizia kwa kusema kuwa Jiji litakuwa linaingiza zaidi ya sh. bilioni 1 kwa mwaka kutokana na tozo mbalimbali.

No comments:
Post a Comment