![]() |
| Waziri wa Madini ,Doto Biteko, akizungumza juu ya mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan. |
![]() |
| Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini taarifa ya mafanikio mwaka mmoja ya Serikali ya awamu sita katika sekta ya Madini ikisomwa na Waziri wa Madini Doto Biteko |
Na,Okuly Julius, Dodoma
Chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umekuwa ukiongezeka kutoka robo moja ya mwaka hadi nyingine Katika kipindi cha Januari - Septemba.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Madini Mheshimiwa Doto Biteko wakati akiwasilisha ripoti ya mwaka mmoja ya wizara hiyo ambapo amesema kuwa,2021 wastani wa mchango wa sekta hii umekua hadi kufikia asilimia 7.3 ya Pato la Taifa ikilinganishwa na wastani wa asilimia 6.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2020.
Aidha, katika robo ya tatu (Julai -Septemba) mwaka 2021,mchango wa sekta ya madini umeongezeka hadi kufikia asilimia 7.9 ya Pato la Taifa kutoka asilimia 7.3 ya Pato la Taifa katika kipindi kama hicho mwaka 2020.
Amesema kuwa Matokeo haya yanaakisi dhamira ya Serikali kuhakikisha sekta hii inaimarika na kuweza kuchangia Pato la Taifa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025 kama ilivyotangazwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa na Mpango wa Maendeleo.
Kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa serikali ya awamu ya sita sekta ya madini imeweka historia kwa kushuhudia mauzo ya moja kwa moja yenye thamani ya Shilingi Trilioni 8.3 kutokana na mauzo ya madini ya aina mbalimbali.
Mauzo hayo yanatokana na madini ya dhahabu, madini ya fedha, madini ya shaba, makaa ya mawe, madini ya kinywe, madini ya vito na madini ya ujenzi na viwandani ambapo Kutokana na biashara ya madini hayo, Wizara imekusanya Shilingi Bilioni 597.53 kama maduhuli ya Serikali yaliyokusanywa kupitia Wizara yetu.
Vile vile Mheshimiwa Waziri Biteko ameongeza kuwa ushiriki wa Watanzania kwenye shughuli za madini umekuwa kutoka asilimia 48 hadi asilimia 63 na hivyo kuongeza thamani ya huduma migodini kufikiai thamani ya Dola za Marekani Milioni 579.3 sawa na Shilingi Trilioni 1.33 kutokana na huduma zilizotolewa migodini.
Pia amebainisha kuwa kwa sasa Wizara imeongeza usimamizi kwenye madini ya ujenzi na viwandani ambapo tayari mifumo ya kielekronik imeanza kutumika katika usimamizi wa mapato ya Serikali yatokanayo na madini hayo.
Katika juhudi za kusimamia upatikanaji wa mapato kutokana na madini ya ujenzi na viwandani, Wizara ya Madini imeanza ushirikiano na Wizara ya TAMISEMI ili kuweza kuwafikia wananchi wanaotumia madini hayo waweze kuchangia fedha zitokanazo na shughuli za uchimbaji madini hayo kwa mujibu wa Sheria ya Madini.
Pamoja na hayo Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhesimiwa Samia Suluhu Hasan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kusimamia na kuhakikisha wachimbaji wadogo wanashiriki kikamilifu na kwa ufanisi kwenye uzalishaji madini hapa nchini, Katika usimamizi huo, kwa sasa wachimbaji Wadogo wanachangia zaidi ya asilimia 30 kwenye mapato yatokanayo na madini.
Matokeo na mafanikio hayo yanatokana na jitihada mbalimbali za Serikali ya awamu ya sita ikiwa ni pamoja na kuimarisha Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini.Katika kuimarisha taasisi hizo.Senkali imewezesha ushiriki wa taasisi katika maonesho na shughuli mbalimbali za kutangaza fursa na shughuli zinafanywa taasisi hizo kupitia Wizara ya Madini.
Hivyo kupitia,Maonesho Makubwa ya Biashara ya Dubai Expo2020 Serikali kupitia STAMICO hivi karibuni imesaini mkataba wa uchorongaji kati yake na Buhemba Gold Company wenye thamani ya shilingi bilioni 11.5.
Aidha, STAMICO imeendelea kuwa mlezi wa wachimbaji wadogo ili hatimaye waweze kukua na kuongeza tija katika kufanya shughuli zao. Katika kutekeleza hii. STAMICO imesaini mikataba na benki mbalimbali za biashara nchini kwa ajili ya kuwasaidia wachimbaji wadogo kupatiwa mikopo na kuwaunganisha na benki
Huku akibainisha kwamba kwa sasa ipo tofauti kubwa sana kati ya STAMICO ya sasa na ya zamani kutokana na matokeo makubwa ambayo shirika hili linaendelea kufanya.
Kupitia juhudi hizi, Shirika lilifanikiwa kukusanya shilingi bilioni 19.97 kati ya Machi 2021 na Februari 2022 kutoka vyanzo vyake vya ndani.
Kwa upande wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), katika kuhakikisha inatimiza malengo yake ipasavyo, imefanikiwa kusogeza karibu na wachimbaji wadogo wa madini huduma za maabara kwa lengo la kuwasaidia wachimbe kisayansi na hivyo kuongeza tija na mapato ya serikali.
Tayari Ofisi hizo zimefunguliwa katika mkoa wa Geita na lengo ni kuendelea kufungua ofisi hizi kwenye kanda zenye shughuli nyingi za uchimbaji madini. Aidha,huduma za maabara na utafiti zimeboreshwa zaidi kwa GST kupatiwa mashine mbalimbali za kisasa za uchunguzi wa madini na tafiti za jiosayansi zikiwemo Tanuru kubwa na la kisasa la uchunguzi wa sampuli za dhahabu lenye uwezo wa kufanya uchunguzi wa sampuli 50 kwa mkupuo kwa muda wa saa moja ukilinganisha na uwezo wa sampuli 16 kwa mkupuo kwa muda wa saa moja kwa tanuru lililokuwepo



No comments:
Post a Comment