Bodi ya wataalam wa ununuzi na ugavi ( PSPTB ) wametangaza matokeo ya mtihani wa 23 ya kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi.
Akitangaza matokeo hayo jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi amesema kuwa jumla ya Wadahiliwa walikuwa 479,kati yao waliofanikiwa kufanya mitihani ni 427 ambapo 28 kati yao hawakufanya kabisa mtihani huo.
Pamoja na hayo Godfred Mbanyi amesema kuwa wanafunzi 65 wamefeli kabisa ambapo ni sawa na asilimia 14.4% hivyo wanatakiwa kurudia mitihani hiyo katika ngazi ambazo walirisiti kufanya mitihani hiyo huku akielezea kuwa kila ngazi inakuwa na mitihani minne hivyo hawa waliofeli wanapaswa kurudia mitihani yote.
Pia watahiniwa 230 wanatakiwa kurudia baadhi ya mitihani waliyofeli (Suplimentary) ili kukidhi ufaulu katika masomo waliyofeli.
Ameongeza kuwa katika mitihani mingi ya Bodi inayohusiha maswala ya mahesabu ,takwimu, Uchumi na masomo mengine yenye kuhusisha hesabu wanafunzi wamekuwa wakifanya vibaya huku akizungumzia pia mitihani ya kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi kuna wanafunzi pia wamefeli hivyo wanapaswa kufanyia kazi kwa sababu ndio maeneo ambayo watakwenda kufanyia kazi.
Amesema jumla ya Masomo ni 32 huku akisema kati ya hayo Masomo 6 wamefanya vibaya sana ,17 ni ufaulu wa Wastani na masomo 11 wamefanya vizuri kiasi na kufanya jumla ya wastani wa ufaulu katika mitihani hiyo ya Bodi ya kataalamu ya Ununuzi na Ugavi kuwa ni asilimia 34.6% kwa mitihani hii ya 23.
Aidha,amewataka wanafunzi wote waliofeli mitihani na wale wanaotakiwa kurudia kuhakikisha wanajisajili tena kwa ajili ya kufanya mitini hiyo.
Amemalizia kwa kutangaza rasmi kuwa kwanzia Jumatatu ya tarehe 14 ,March 2022 dirisha litakuwa wazi kwa ajili ya wanafunzi watakaohitaji kufanya mitihani hii ya bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi ambapo fomu za kujiunga zitapatikana katika tovuti ya bodi hivyo usajili wote utafanyikia mtandaoni (Online) na kuwataka wanafunzi kujiyokeza kwa wingi kuomba nafasi hiyo ya kufanya mitihani ya Kitaaluma ya ununuzi na ugavi.



No comments:
Post a Comment