Ikumbukwe kuwa Simba SC tayari wametanguliza kifua Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma lililopita.
Bao pekee la Simba inayofundishwa na kocha Mspaniola, Pablo Franco Martin lilifungwa na beki mkongwe wa kulia, Shomari Salum Kapombe kwa penalti dakika ya 68.
Penalti hiyo ilitolewa na refa Mtunisia, Haythem Guirat baada ya winga Mghana, Bernard Morrison kuwekwa chini kwenye boksi.
Timu hizo zitarudiana leo Jumapili kuanzia majira ya saa moja usiku katika Uwanja wa Orlando Jijini Johannesburg.
Simba itakosa huduma ya winga Mghana, Bernard Morrison ambaye amefungiwa kuingia nchini Afrika kusini.




No comments:
Post a Comment