![]() |
Mjiolojia Mwandamizi wa GST John Kalimenze , akitoa elimu juu ya Matetemeko ya ardhi Kwa wakazi wa maeneo ya Ulowa. |
![]() |
Mjiolojia Mwandamizi wa GST John Kalimenze , akitoa elimu juu ya Matetemeko ya ardhi Kwa wakazi wa maeneo ya Ulowa. |
Na Samwel Mtuwa ,Kahama
Kufuatia kuwepo kwa taarifa za kutokea kwa mitetemo ya ardhi ambayo ilisababisha TAHARUKI kubwa katika maeneo ya Ulowa Wilayani Ushetu/Kahama, Wataalamu kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) walifika katika eneo hilo na kutoa elimu kuhusu namna bora ya kuchukua tahadhari ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mitetemo ya ardhi.
Akiongea katika hadhara hiyo ya wananchi wa Ulowa namba 8, Mjiolojia Mwandamizi kutoka GST Bw. John Kalimenze, aliwaeleza wananchi kwamba tetemeko la ardhi ni mojawapo ya majanga ya asili ya jiolojia ambayo yanatokana na nguvu za asili zinazosababishwa na mabadiliko ya jiolojia na hivyo yanaweza kutokea wakati wowote.
Kwa bahati mbaya duniani kote, hakujapatikana teknolojia ya kubaini tetemeko litatokea lini, hivyo tunapaswa kuchukua tahadhali muda wote.
Aidha, Bw. Kalimenze aliwaeleza wananchi kwamba nchi yetu imepituwa na ukanda wa bonde la ufa likiwa na mikondo miwili; mkindo wa Mashariki na mkondo wa Magharibi ambapo matukio ya matetemeko ya ardhi ni dhahiri kutokea. Bw. Kalimenze alifafanua kwa kina kuhusu hatua za tahadhari za kabla ya tukio, wakati wa tukio na baada ya tukio la tetemeko la ardhi.
Akiongea kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ulowa namba 8 Ndg.Charles Moses Mihambo aliishukuru sana Serikali kwa kuealeta wataalamu wa GST kufika mapema kwa lengo la kutoa elimu kuhusu matetemeko ya ardhi ili kuondoa TAHARUKI kubwa na sintofahamu iliyokuwepo kwa wananchi wa Ulowa.
Mwenyekiti aliomba taasisi ya GST kuendelea kutoa elimu ya matetemeko na kwamba mpango huo wa kutoa elimu uwe endelevu ili kuwajengea wananchi uelewa mpana wa namna ya kuchukua tahadhari.
No comments:
Post a Comment