![]() |
Mmoja wa Wakurugenzi wa TAN PORT WINE Ndugu Clement Paul akionesha bidhaa zao katika maonesho yanayoendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma |
![]() |
Mmoja wa Wakurugenzi wa TAN PORT WINE Ndugu Clement Paul akionesha bidhaa zao katika maonesho yanayoendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma |
Na Okuly Julius Dodoma
Maadhimisho ya usalama na afya mahali pa kazi yanaendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete lengo kubwa la maadhimisho hayo ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu mahala pa kazi.
Kiwanda cha kutengeneza Mvinyo cha TAN PORT WINE kilichopo eneo la viwanda Kizota katika magodaoni ya Sido ambao pia wameweka banda lao katika viwanja hivyo , kupitia mmoja wa Wakurugenzi wake Ndugu Clement Paul amesema kuwa kiwanda chao kimeanza rasmi mwaka 2017 kwa kuzalisha lita 1,000 ila mpaka mwaka huu 2022 wanazalisha zaidi ya lita elfu 40,000 ambapo Mvinyo wao wanausindika takriban mwaka mmoja.
Ambapo kutokana na usindikaji huo Clement Paul amesema kuwa MVINYO kutoka TAN PORT WINE ni bora na wenye viwango vikubwa kwa sasa hivyo kwa wenye shughuli zao wachukuwe na kutumia hakika hawatajutia.
"Mvinyo wetu ni bora sana na ladha yake ni inasisimua sana kikubwa ninachofurahia ni jinsi ambavyo tunaandaa mpaka kumfikia mtumiaji"Amesema Clement Paul
Pia Clement ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo wamepata fursa ya kutangaza zaidi bidhaa zao na kufanya watu wengi kuwafahamu na hilo ni moja kati ya mambo ya kujivunia katika maonesho hayo.
"Sisi kama TAN PORT WINE tumekuwa wanufaika wakubwa wa maonesho haya pamoja na hayo tumejifunza mbinu nyinginezo za kuhakikisha tunawakea wafanyakazi wetu mazingira salama katika maeneo yao ya utendaji na Afya zao ziwe salama ndio faida pia itaonekana kwa kiwanda chetu" Amesema Clement Paul .
Kilele cha Maonesho hayo ni April 28 ,2022 na mgeni rasmi Mhe.Prof Joyce Ndalichako Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Ikumbukwe kuwa maonesho hayo nchini yalianza kuadhimishwa tangu mwaka 2004 ambapo maadhimisho hayo yamekuwa yakiratibiwa na Serikali kupitia Taasisi yake ya OSHA kwa kushirikiana na Wadau wa Utatu ambapo ni Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi- TUCTA na Chama cha Waajiri Tanzania- ATE pamoja na Shirika la Kazi Duniani-ILO.
![]() |
kwa Mawasiliano zaidi wapigie kupitia nambari za simu hapo juu kama una shughuli yako unaweza kusindikiza na Mvinyo safi kabisa kutoka TAN PORT |
No comments:
Post a Comment