Na Okuly Julius-Dodoma
Ambapo Tangu tarehe 9 Mei, 2022 mwenendo wa uombaji wa kazi za muda za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 unaendelea kwa kasi kubwa ikilinganishwa na wiki ya kwanza ya tangazo lilipotolewa.
Ameongeza kuwa Mafanikio hayo yanatokana na changamoto zilizotolewa na kufanyiwa kazi na Serikali kwa wakati jambo ambalo limeongeza kasi ya uombaji ambapo mpaka kufikia tarehe 16Mei,2022 ofisi ya tifa ya Takwimu imepokea jumla ya maombi 532,347 ambapo linakuwa ni ongezeko la maombi 412,879 ndani ya kipindi cha siku saba.
"Hadi kufikia leo tarehe 16 Mei, 2022 saa saba kamili mchana, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imepokea jumla ya maombi 532,347 kati ya nafasi 205,000 zinazohitajika ikilinganishwa na maombi 119,468yaliyokuwa yamepokelewa na kutangazwa kwa Umma tarehe 9 Mei, 2022 saa saba kamili mchana. Hili ongezeko la maombi 412,879 ndani ya kipindi cha siku saba" Amesema Bi.Ruth Minja
Amebainisha kuwa Kati ya maombi 532,347 yaliyopokelewa hadi sasa, waombaji 193,548 (asilimia 36) ni waajiriwa kutoka katika sekta ya umma na binafsi; waombaji 58,566 (asilimia 11) wamejiajiri wenyewe na waombaji 280,233 (asilimia 53) ni wale ambao hawana ajira.
Pia Bi.Ruth Minja ametoa wito kwa wanaotuma maombi ya ukarani au usimamizi wa maudhui au usimamizi wa TEHAMA wafuate kwa ukamilifu maelekezo yaliyowekwa kwenye Tangazo la Kazi; wajaze Fomu ya Maombi kwa ukamilifu na waambatanishe nyaraka zote muhimu zinazohitajika.
Aidha, mwombaji anatakiwa ahakikishe anajaza namba ya simu na barua pepe ambayo anaitumia kwa sasa ili aweze kupokea taarifa za akaunti yake ya kuingia kwenye mfumo ili kukamilisha kutuma maombi ya kazi.
No comments:
Post a Comment