Carlo Ancelotti kuweka historia leo? Ama atavutwa shati na Majogoo? Fainali Ligi ya Mabingwa mjini Paris - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 28, 2022

Carlo Ancelotti kuweka historia leo? Ama atavutwa shati na Majogoo? Fainali Ligi ya Mabingwa mjini Paris



Maelfu ya mashabiki wa kandanda wanamiminika katika mji wa Paris kutizama fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid na Liverpool itakayochezwa baadae leo katika uwanja wa Stade de France.

Carlo Ancelotti analenga kuwa kocha wa kwa kwanza kushinda kombe hilo la Ulaya mara nne, akiongeza kwenye mafanikio yake ya 2014 wakati alipokuwa na Real Madrid kwa mara ya kwanza.

Muitaliano huyo alishinda mataji mawili ya kwanza ya Ulaya akiwa na AC Milan mwaka wa 2003 na 2007.

Liverpool ilishinda ubingwa wake wa Ulaya kwa mara ya sita katika fainali ya 2019 kwa kuifunga Tottenham Hotspur 2- 0.

Vijana hao wa kocha Mjerumani Jurgen Klopp wanaweza kumaliza msimu huu wakiwa na mataji matatu. Tayari walishinda Kombe la FA na Kombe la EFL.


No comments:

Post a Comment