FANYENI BIASHARA KWA UHAKIKA, WAZIRI MKUU AWAAMBIA WAMACHINGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 25, 2022

FANYENI BIASHARA KWA UHAKIKA, WAZIRI MKUU AWAAMBIA WAMACHINGA



 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wafanyabiashara ndogondogo na wajasiriamali wafanye biashara zao kwa uhakika kwa sababu Serikali inataka watimize matananio yao. 

 “Serikali hii inawatambua na itasimamia matamanio yenu na mtafuika kwenye ndoto zenu. Mtaji uliowekezwa kwenye vibanda hivi na Jiji ni shilingi bilioni moja na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akaongeza shilingi milioni 500 ili masoko mengi yajengwe,” amesema.

 Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Arusha kwa ziara ya siku moja, amekagua masoko ya Mbauda, Kilombero na Machame na kuzungumza na baadhi ya wamachinga wanaofanya biashara kwenye masoko hayo.

 Akizungumza kwa nyakati tofauti na wajasiriamali hao baada ya kukagua kila soko  (Jumanne, Mei 24, 2022), Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo wakue kimitaji na kumiliki biashara kubwa.

 "Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan nia yake ni kuwafanya muweze kuwa na maeneo yanayotambulika, kisha mpate kipato rasmi ili nanyi muwe wafanyabiashara wakubwa hapo baadaye. Hapa Arusha wako wafanyabiashara maarufu ambao walianza kwa kusafisha viatu lakini leo wanamiliki biashara kubwa kubwa," amesema.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alipomtaka Meneja wa TANESCO wa wilaya, Bw. Amiri Chambua aseme ni lini wataweka umeme, Bw. Chambua aliahidi kukamilisha kazi hiyo kesho (Jumatano, Mei 25, 2022). Alikiri kupokea barua ya maombi tangu mwezi uliopita na kudai kwamba walikuwa kwenye mchakato wa maandalizi.

Kuhusu kadhaa ya askari mgambo, Waziri Mkuu amewataka watumie weledi na maarifa kwenye kazi yao ya ulinzi. “Mtu kama anauza eneo lililoruhusiwa, askari tumieni miongozo na waeleweshwe; na pia zile mali mlizoweka kule Depot warudishieni kwa sababu mitaji ni midogo,” alisema na kuamsha shangwe miongoni mwa wafanyabiashara hao.



No comments:

Post a Comment