SHEKH Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mustafa Rajab  amewataka waumini wa Dini ya Kiislamu kuendeleza matendo mema hata baada ya mfungo - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, May 3, 2022

SHEKH Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mustafa Rajab  amewataka waumini wa Dini ya Kiislamu kuendeleza matendo mema hata baada ya mfungo


SHEKH Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mustafa Rajab 

NA JOHN BANDA, DODOMA

SHEKH Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mustafa Rajab amewataka waumini wa Dini ya Kiislamu kuendeleza matendo ya unyenyekevu, kusaidia wasiojiweza na kutotenda dhambi za aina yoyote kama walivyofanya wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Akiongea wakati alipokuwa akitoa mawadha katika ibada ya Eid al Fitry iliyofanyika katika msikiti wa Gadafi jijini Dodoma Rajab amesema mfungo umekwisha lakini haimaanishi watu wakatende matendo ya kumchukiza mwenyezi Mungu

Shekh huyo amesema kila muislam amejitahidi katika mwezi mtukufu wa Ramadhan kufunga na kutenda matendo yaliyoagizwa na Mungu hivyo inabidi kila mmoja ahakikishe hatendi dhambi

“niwaase waislam wenzangu kuwa ni vizuri kuyaendeleza yote ambayo tulikuwa tukiyafanya wakati wa mfungo ambapo hatukutenda dhambi, tuliishi kwa unyeyekevu na kuwasaidia wenzetu wasiojiweza maana hiyo ndiyo ibada Mungu anaipenda na hakika atatupa thwawabu”, alisema

Aidha aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi wakati wa sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi wa 8 mwaka huu

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa sherehe za waislam mkoani Dodoma Shekh Yusufu Husein Said akiongea katika uwanja wa jamhuri jijini humo amesema Mungu aliyekuwepo Wakati wa mfungo wa Ramadhan ndiye anayeendelea kuwepo na miezi mingine yote

“tusijisahau Mungu tuliyemuomba kwa unyenyekevu na kutenda matendo mema wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan anaendelea kuwepo hivyo tudumishe matendo mema ya kumpendeza mwenyezi Mungu”, alisema

Safari ya mfungo huo wa Ramadhani umehitimishwa kwa waislamu kukamilisha nguzo ya 5 kati ya nguzo 6 ambapo kila mwenye uwezo akitakiwa kushiriki Zakaliftily ambapo hutakiwa kutoa zaka ambazo huelekea kuwasaidia wasiojiweza ambapo kwa msikiti huo wamepangia kutoa chakula kuanzia kilo 2 na kuendelea


No comments:

Post a Comment