Chakula Bora kwa Uzazi wa Mwanamke - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 18, 2022

Chakula Bora kwa Uzazi wa Mwanamke



Kula kwa afya ina maanisha kupata vyakula tofauti tofauti kutoka katika makundi tofauti ya vyakula. Jaribu kujumuisha yafuatayo katika mlo wako wa kila siku:
.
✅Angalau sehemu tano ya matunda na mboga za majani. Matunda na juisi ya mbogamboga na juisi laini (smooth) zinajumuishwa kwenye sehemu hizi. Kumbuka kwamba juisi zinakua na sukari nyingi hivyo jaribu kuepuka na hakikisha unapata150ml ya glasi kwa siku.
.
✅Zingatia mlo wa nafaka zisizokobolewa na viazi ambavyo vitakupatia wanga na kabohaidreti pamoja na fiba (fibre, pia vitamini na madini kwa wingi yenye umuhimu.
✅Hii inajumuisha mkate wa ngano usiokobolewa, mchele wa kahawia, nafaka zisizokobolewa na tambi.
.
✅Jumuisha vyakula vya protini katika kila mlo, kama vile nyama, samaki, mayai na maharage. Jaribu kula angalau mara mbili samaki kwa wiki.
✅Mojawapo ya samaki hawa awe wa mafuta, lakini usile zaidi ya mara mbili kwa wiki samaki wa aina hii.
.
✅Baadhi ya vyakula vya maziwa vilivyo na kalsiamu, kama maziwa, mtindi na jibini. Lenga kula mara mbili mpaka tatu kwa siku. Kama uko makini kwenye idadi ya kalori, jaribu kuchagua vyakula vyenye kalori ndogo au zisizo na fati au sukari.
.
✅Baadhi ya vyakula vyenye wingi wa madini chuma kama nyama nyekundu,matunda, mkate, mboga za kijani na nafaka zisizokobolewa. Hizi hujenga wingi wa madini chuma na kukuandaa kwa ujauzito.

Kwa ushauri zaidi unaweza ukapiga simu kwa namba zifuatazo +255 687 699 598

No comments:

Post a Comment