Urusi yamhukumu mwalimu wa Marekani miaka 14 kwa kusafirisha bangi - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 18, 2022

Urusi yamhukumu mwalimu wa Marekani miaka 14 kwa kusafirisha bangi



Mahakama ya Urusi imemhukumu mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani kifungo cha miaka 14 jela kwa kosa la ulanguzi wa bangi.

Marc Fogel hapo awali alikuwa akifanya kazi katika ubalozi wa Marekani huko Moscow, lakini aliajiriwa kama mwalimu wa Kiingereza katika jiji hilo wakati wa kukamatwa kwake.

Fogel alihukumiwa katika mamlaka ambayo inasikiliza kesi inayohusiana na bangi dhidi ya nyota wa mpira wa vikapu wa Marekani Brittney Griner.

Bangi ni halali katika maeneo mengi ya Marekani, lakini bado ni haramu nchini Urusi.

"Raia wa Marekani Fogel amepatikana na hatia," mahakama katika kitongoji cha Moscow cha Khimki ilisema katika taarifa.

Taarifa hiyo ya habari ilisema kuwa mwalimu huyo wa Kiingereza alikuwa amefanya "usafirishaji wa dawa za kulevya kwa kiwango kikubwa" pamoja na "uhifadhi mkubwa haramu wa dawa bila malengo ya kibiashara".

Fogel, ambaye ana umri wa miaka 60, alikuwa na takriban 17g (0.6oz) ya bangi kwenye mzigo wake aliponaswa tarehe 15 Agosti 2021 kwenye uwanja wa ndege wa Sheremetyevo, aliwaambia mawakili.

Mamlaka za mitaa hazijatoa maoni juu ya kiasi cha madawa ya kulevya ambayo Fogel alikuwa amebeba, lakini sheria ya Urusi inafafanua "kiasi kikubwa" cha bangi kuwa angalau 100g.

Fogel alisema daktari aliagiza dawa hiyo kwa sababu za kiafya baada ya kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo, na kwamba hakufahamu kwamba bangi inayotumiwa kwa matibabu ni kinyume cha sheria nchini Urusi.

Alikubali hatia ya kusafirisha, kuhifadhi, kutengeneza na kusindika dawa za kulevya, kulingana na shirika la habari la Urusi la Interfax, na alihukumiwa kutumikia kifungo chake katika koloni yenye ulinzi mkali.

Kama sehemu ya uchunguzi, polisi walitoa picha za upekuzi uliofanywa na wachunguzi katika Shule ya Anglo-American huko Moscow, ambapo Fogel alikuwa akifanya kazi.

Hukumu yake inajiri siku mbili baada ya mahakama ya Khimki kuchelewesha kesi ya Bi Griner tena.

Nyota huyo wa Phoenix Mercury alizuiliwa Februari mwaka jana kwa madai ya kubeba mafuta ya bangi nchini humo.

Raia kadhaa wa Marekani kwa sasa wako katika jela za Urusi, akiwemo mwanajeshi wa zamani wa Marekani Paul Whelan, ambaye alihukumiwa mwaka 2020 kutumikia kifungo cha miaka 16 kwa kosa la ujasusi. Marekani pia ina raia kadhaa wa Urusi gerezani.

Mwezi Aprili, nchi hizo mbili zilikubaliana kubadilishana wafungwa ambapo aliyekuwa Mwanamaji wa Marekani alibadilishwa na rubani wa Urusi ambaye alikuwa amefungwa jela tangu 2010.


No comments:

Post a Comment