Mshambulizi wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, anatazamia kuondoka Manchester United, huku Roma ya Jose Mourinho na Sporting Lisbon zikivutiwa naye . (La Repubblica, in Italian, subscription needed)
Arsenal wana "matumaini makubwa" ya kumsajili fowadi wa Manchester City Mbrazil Gabriel Jesus, 25. The Gunners wanatumai pauni milioni 30 zitatosha lakini City wanataka pauni milioni 50. (Sky Sports)
The Gunners bado wanaweza kumsajili kiungo wa Leicester Ubelgiji Youri Tielemans, 25, licha ya kuwa wanatazamiwa kukamilisha dili la kiungo mwingine wa Porto Fabio Vieira, 22, ambaye ni Mreno. (Evening Standard)
Arsenal pia inamtaka winga wa Leeds Mbrazil Raphinha, 25, na mlinzi wa Ajax Muajentina Lisandro Martinez, 24. (Athletic, subscription needed)
Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel angependa kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29 - ambaye analengwa na Inter Milan - na mshambuliaji wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 33 wa Poland Robert Lewandowski, lakini kuna vikwazo muhimu katika kukamilisha mikataba yote miwili. (ESPN)
Lewandowski anayelengwa na Barcelona anasema bado anataka kuondoka Bayern lakini hataki kuharibu uhusiano wake na klabu hiyo ya Ujerumani kwa kulazimisha uhamisho (Express)
Tottenham wapo mstari wa mbele kumsajili mlinzi wa Middlesbrough Muingereza Djed Spence, 21, huku Nottingham Forest ikikubali kuwa huenda asijiunge nao, baada ya kukaa kwa mkopo City Ground msimu uliopita. (Northern Echo)
Manchester United wana imani Barcelona itapunguza bei yao ya pauni milioni 73 ili kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, kwa sababu ya matatizo yao ya kifedha. (Guardian)
West Ham wako tayari kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa Croatia Nikola Vlasic, 24, huku Hadjuk Split na Torino wakimtaka. (Dalmatinskiportal, in Croatian)
Sevilla wako tayari kutoa £6.9m kwa mshambuliaji wa Rangers na Colombia Alfredo Morelos, 25. (Fichajes, in Spanish)
Fulham wako tayari kukamilisha usajili wa pauni milioni 7 wa mshambuliaji wa Israel Manor Solomon, 22, kutoka Shakhtar Donetsk. (Sun)
Mshambulizi wa Watford wa Nigeria Emmanuel Dennis, 24, yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na Everton msimu huu ikiwa fowadi wao wa Brazil Richarlison, 25, ataondoka. (Mail)
Nottingham Forest wanakaribia kumnunua mlinzi wa Mainz Mfaransa Moussa Niakhate, 26. (Football Transfers)
Southampton wana matumaini ya kumsajili beki wa Marekani wa Bayern Munich Chris Richards, 22. (GiveMeSport)
Celtic wanakabiliwa na pambano jipya kutoka kwa Ajax katika vita vya kumnasa kiungo wa kati wa Lommel wa Brazil Vinicius Souza, 22. (Record)
Paris St-Germain wanatazamiwa kuzishinda timu kadhaa za Premier League hadi kufikia pauni milioni 34 kumsajili kiungo wa kati wa Porto Mreno Vitinha, 22. (90min)
Hibernian inatazamiwa kumsajili winga wa zamani wa Sunderland na Jamhuri ya Ireland Aiden McGeady, 36, kwa uhamisho wa bure. (Record)
No comments:
Post a Comment