Umoja wa askari Polisi Mkoa wa Dodoma (J1) waliotimiza miaka kumi ya utumishi kazini wamesherehekea siku hiyo kwa kufanya matendo ya huruma katika kituo cha kulelea watoto wenye uhitaji Tupendane kilichopo Kikuyu Jijini hapo.
Akiongoza zoezi Hilo Septemba 18,2026 Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Dodoma ASP Regina Mtana amesema Jeshi la Polisi ni sehemu ya Jamii hivyo hushirikiana na wananchi katika mambo mbalimbali ikiwemo shughuli za kimaendeleo.
Msaada huu wa askari Namba J1 ni sehemu ya kipato Chao hivyo kupitia mahitaji walioleta na mapenzi walionesha Kwa watoto hao itasaidia kuwapa faraja na kufanya vizuri katika masomo.
Vilevile Mtana amesema mbali naJeshi la Polisi kutekeleza majukumu ya ulinzi na usalama kwa wananchi pia askari kupitia umoja wao walionao na depo mbalimbali wamekuwa na utaratibu wa kufanya matendo ya huruma Kwa wenye uhitaji, kushiriki katika shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira na kufanya matendo ya huruma.
Vilevile katibu wa umoja askari Namba (J1) Mkoa wa Dodoma James Boymanda amesema wamekuwa na utaratibu wa kufanya jambo hilo mara kwa mara ikiwa ni sehemu ya kuongeza umoja na mshikamano kwa Jamii na kuwawezesha watoto wenye uhitaji kufikia malengo yao.
Uongozi wa kituo hicho umepongeza Jeshi la Polisi kupitia umoja wa askari hao kusherehekea sikukuu hiyoKwa kuikumbuka Jamii na kuwawezesha baadhi ya mahitaji ambayo yalikuwa ni changamoto ikiwemo vifaa vya mashuleni na kuitaka Jamii kutembelea kituo hicho na kuwafariji watotoa hao.
















No comments:
Post a Comment