Na WMJJWM, DODOMA.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula ameiasa jamii kuwekeza kwenye malezi na makuzi sambamba na kuwaepusha watoto na Ukatili.
Akizungumza na kikosi kazi cha Utekelezaji wa Programu jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, MMAM (2021/2022 -2025/2026) iliyozindiliwa kwa lengo la kuhakikisha Watoto wote Tanzania wapo katika mwelekeo sahihi kufikia ukuaji timilifu, Dkt Chaula amesisitiza wanajamii kushiriki kikamilifu kuhakikisha watoto wanalindwa.
“Watoto hawa wanategemewa na Taifa letu na ndiyo watakao tutunza hapo baadae sisi tukishazeeka, hivyo wito wangu kwa jamii ni kujiepusha na Matendo ya kikatili yanayowakumba watoto”alisema Dkt Chaula.
Amesema kikosi kazi hicho cha kitaifa kimeundwa kwa ajili ya kutoa ushauri na ufuatiliaji wa karibu kuhusu malezi na Makuzi kwa watoto kwa muda wa miaka minne na hiyvo wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano.
Naye Mkurugenzi wa Mtandao wa Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mwajuma Rwebangila ameishukuru Serikali kwa kutoa mwongozo na ushirikiano kuanzia hatua ya uandaaji wa Programu hii hadi sasa Utekelezaji wake umeanza.
Utelekezaji wa Programu hii Jumuishi unasimamiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Wizara ya Mambo ya Ndani,Wizara ya Afya Pamoja Na Wizara ya Fedha na Mipango.
No comments:
Post a Comment