VIDEO ,TUNA JUKUMU LA KUTUNZA RASILIMALI ZA MAJI -AWESO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 30, 2022

VIDEO ,TUNA JUKUMU LA KUTUNZA RASILIMALI ZA MAJI -AWESO

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati akizindua Bodi ya Nne ya Maji ya Taifa leo jijini Dodoma juni 30,2022
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikata utepe wakati akizindua Bodi ya nne ya maji ya taifa hafla iliyofanyika leo juni 30,2022 jijini Dodoma wa pili kulia ni naibu waziri wa Wizara hiyo Marryprisca Mahundi na kushoto ni Katibu mkuu wa wizara hiyo Eng.Anthoni Sanga

Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri wa Maji Mh Jumaa Aweso ameitaka Bodi ya Nne ya Maji ya Taifa kuwa wabunifu,kulinda Mitambo ya Maji pamoja na kulinda Rasilimali za Maji ili kuongeza wigo wa kupeleka Huduma ya Maji kwa Wananchi.

Akizindua Bodi ya Nne ya Maji ya Taifa leo jijini Dodoma Mh jumaa Aweso amesema kuwa Rasilimali za Maji ndiyo moyo katika kufanya Mageuzi Makubwa ya kiuchumi.

Aidha.Mh Aweso amesema kuwa ili wizara ya Maji iweze kufanikiwa katika suala zima la ulindaji na usimamizi wa Rasilimali za Maji ni lazma kuwashirikisha viongozi na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Nne ya Maji ya Taifa Eng.Mbogo Futakamba ameithibitishia serikali kuwa watafanya kazi kwa juhudi,weledi na Maarifa.


No comments:

Post a Comment