DKT CHAULA AKUTANA NA MWAKILISHI MKAAZI WA UN WOMEN  - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 17, 2022

DKT CHAULA AKUTANA NA MWAKILISHI MKAAZI WA UN WOMEN 

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Mkaazi wa UN Women hapa nchini Bi.Hodan Addou ( kushoto) katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula (katikati) akisalimiana na Mwakilishi Mkaazi wa UN Women hapa nchini Bi.Hodan Addou ( kushoto) pamoja na naibu katibu wa wizara hiyo Amon Mpanju (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dodoma.

   Na Mwandishi wetu Dodoma 

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amekutana na Mwakilishi Mkaazi wa UN Women hapa nchini Bi.Hodan Addou katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Dkt. Chaula na Bi.Hodan wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo uwezeshaji Wanawake kiuchumi Usawa wa Kijinsia na mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili.

Kikao hicho pia kilihudhuliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju na wataalam wengine wa Wizara.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kukutana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mikakati ya Wizara katika kuhudumia wananchi kupitia Wizara hiyo mpya.

No comments:

Post a Comment