Na Okuly Julius Dodoma
ZOEZI la Uchangiaji wa damu wa hiari wa kujirudia unahitajika ili kuhakikisha damu inapatikana kwa wanaotakiwa kuongezewa damu dharura zinapojitokeza.
Ukichangia damu unaonyesha mshikamono na pia unatoa zawadi ya uhai kwa mtu anayehitaji damu katika jamii yako.
Akizungumza wakati akifunga kilele cha uchangiaji damu Salama kwa mkoa wa Dodoma Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr.Samweli Seseja amewataka wananchi kuelewa umuhimu wa kuchangia damu kwani kuchangia damu ni matendo ya Kimungu.
Kama mwananchi unaweza kusaidia uwepo wa damu katika hospitali zetu na kwa muda wote kwa kuchukua kuchangia damu katika kampeni hii na kwa kufanya hivyo utasaidia kuokoa maisha ya mgonjwa mwenye uhitaji wa damu katika jamii.
Dr.Samweli Seseja amesema kuwa Kauli Mbiu ya Siku ya Mchangia Damu Duniani inasema: Kuchangia Damu ni Kitendo cha Mshikamano, Tuungane Kuokoa Maisha (Donating blood is an act of solidarity. Join the effort and save lives) Kauli mbiu hii inaonyesha jukumu la uchangiaji wa damu kwa hiari linavyochangia katika kuokoa maisha ya wahitaji na kujenga umoja ndani ya jamii.
"Kuchangia damu inaleta upendo inajenga amani na inasaidia kuokoa maisha ya watu na jamii inaendelea kuishi ikiwa na afya njema hivyo sisi wwnye afya njema inabidi tutoe damu ili kuweza kuwasaidia wenzetu wenye mahitaji ya damu"Amesema Dr.Samweli Seseja
Na kuongeza ""Hivyo jamii iinabidi ihamasike kuendelea kuchangia damu ili kusaidia wahitaji katika jamii. Kama mwana jamii yatupasa kuona umuhimu wa kujitoa kwa hiari kuchangia damu katika kipindi chote cha mwaka ili kuweza kufanikisha uwepo wa damu ya kutosha kwenye vituo vyetu vya afya"Dr.Samweli Seseja
Kuwashukuru wachangiaji damu na kujenga uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa uchangiaji damu wa hiari wa kujirudia bila malipo.
Kuonyesha umuhimu kwa jamii kujitoa kuchangia damu ili kuweza kuwa na kiasi cha kutosha na salama kwa kipindi chote cha mwaka.
Kutambua na kuhamasisha umuhimu wa uchangiaji damu kwa hiari katika kuimarisha mshikamano kwa jamii.
Kuongea ufahamu/uelewa kwa wadau mbalimbali kuhusu umuhimu/uhitaji wa kuongeza uwekezaji zaidi katika masuala ya damu ili kuboresha na kuweka mifumo madhubuti ya huduma za damu nchini na hatimaye kuongeza kiasi cha damu inayokusanywa kutoka kwa wachangiaji damu wa hiari.
Mahitaji ya damu nchini.
Mahitaji kwa mwaka 2022 ni chupa 550,000 ambayo ni asilimia 1 ya idadi ya wananchi kwa makadirio ya takwimu za mwaka 2020 pia malengo ya mwaka 2022 ni kukusanya chupa 375,000 ambazo ni asilimia 70 ya mahitaji yote.
Mpango wa Taifa wa Damu Salama haujaweza kufikia lengo la kukusanya chupa za damu ambazo zinakidhi mahitaji ya nchi nzima.
Ripoti ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama imeonesha kwa kipindi cha mwaka 2020/2021 kwa kushirikiana na timu za halmashauri wameweza kukusanya chupa za damu 331,279 ambayo ni sawa na asilimia 88% ya lengo na asilimia 60 ya mahitaji ya nchi kwa kutumia vigezo vya WHO (Nchi inahitajika kukusanya damu asilimia 1 ya wakazi wake au chupa 10 kwa kila wananchi 1000. Kwa Tanzania tumefikia chupa 6 kwa kila watu 1000.)
Wahitaji wakubwa wa damu nchini ni pamoja na Watoto chini ya Umri wa miaka mitano ,Kina Mama wakati wa kujifungua ,Wagonjwa wenye Saratani, Sikoseli, Virusi Vya UKIMWI na magonjwa wengine na Wahanga wa ajali
Amefafanua kuwa huduma kwa mchangia damu kabla ya kuchangia damu anapaswa kupima uzito wa mwili,kupima wingi wa damu(Hb),kupima mgandamizo wa damu(Blood Pressure),kupima mapigo ya moyo na ushauri nasaha na kwamba baada ya kuchangia damu vipimo hufanyika maabara za kanda Ili kubaini kundi la damu.
Naye Mhamasishaji wa damu salama na Mhudumu wa Afya ngazi ya jamii wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma Rehema Kassim Mwegeru amezitaja sifa za mtu anaeweza kuchangia damu kuwa ni yeyote, mwanamke au mwanaume mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 65,uzito usiopungua kilo 50 na kwamba kwa mwanamke asiwe mjamzito au anaenyonyesha.
Amesema mwanamke anaweza kuchangia kila baada ya miezi 4 na Mwanamme kila baada ya miezi 3 na kufafanua kuwa uchangiaji damu unawezesha kupima afya bila malipo yoyote, ukichangia damu utapimwa kundi la damu, wingi wa damu, shinikizo la damu, Kaswende na Homa ya Ini B&C
"Uchangiaji damu unapunguza madini chuma mwilini ambapo yakizidi yanaweza sababisha mapigo ya moyo kuongezeka, mwili kujisika kuchoka n,k. Pia kwa kupunguza madini chuma mwilini inasaidia kuzuia uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo na ini,"amesema
Kwa upande wa mchangiaji damu Dotto Faris Mukama amezitaja faida za kuchangia damu ni tendo la upendo na kishujaa, unaokoa maisha ya watu na kwamba Chupa moja inaweza kuokoa maisha ya hadi watu watatu.
Pamoja na hayo amewatoa wasiwasi wengine na kueleza kweli kuhusu kuchangia damu kuwa hakuna madhara yoyote na kwamba , mchangiaji damu hupimwa uzito, wingi wa damu, shinikizo la damu na pia ataulizwa maswali kuhusu maisha ya kila siku.
"Chupa moja ya damu inaujazo wa mililita 450 (ni sawa chupa moja ya soda ya kawaida na zaidi kidogo),asilimia 1 ya watanzania wakiamua kuwa wachangiaji wa damu wa kujirudia uhaba wa damu utaisha.
Pamoja na mambo mengine kauli Mbiu ya Siku ya Mchangia Damu Duniani inasema: Kuchangia Damu ni Kitendo cha Mshikamano, Tuungane Kuokoa Maisha ambayo inaonyesha jukumu la uchangiaji wa damu kwa hiari linavyochangia katika kuokoa maisha ya wahitaji na kujenga umoja ndani ya jamii.
No comments:
Post a Comment