![]() |
Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafunzo wanayotoa katika taasisi hiyo na umuhimu wa ushiriki katika uchumi wa viwanda jijini Dar es Salaam. |
![]() |
Meneja Masoko kampuni ya DIT, Agnes Kimwaga,akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kuwapa nafasi ya kuonyesha bunifu zao katika ofisi zake jijini Dodoma. |
Na Mwandishi wetu Dodoma
Mtaka ameyasema hayo Juni 14,2022 jijini Dodoma wakati wa Maonyesho ya bunifu mbalimbali zilizofanywa na taasisi hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Mtaka, amesema kuwa kumekuwepo na watu ambao wamekuwa wazuri katika kuiba bunifu za watu wengine hivyo kama taasisi hiyo haiatakuwa makini inaweza kujikuta katika wakati mgumu.
“Ni wapaongeze kwa bunifu mnazofanya lakini mnapaswa kuzisajili na kuanza kuzifanyia kazi au kuziuza kwani hizo bunifu ni fedha hamna sababu ya kuendelea kulalamika wakati mmekaa na bunifu kama hizi kwenye makabati”amesema
Mtaka ameichagua taasisi hiyo kufanya kazi kwa wafanyakazi wa bodaboda kwa kutembelea baadhi ya wilaya zilizopo Mkoani humo.
Amesema DIT inauwezo mkubwa katika ufanyaji wa kazi zake na imezalisha wabunifu wengi katika bunifu mbalimbali.
“Mnauwezo mkubwa na ndio maana leo tumewachagua kufanya kazi na Dodoma ambapo kesho mtaanza kuwasajili wanaofanya kazi ya bodaboda”,Amesema Mtaka
“Ubunifu huu umekuwa wa kipekee sana na tunataka tuone mkiendelea kubuni bunifu mbalimbali ambazo nchi nyingine zitaiga kutoka kwetu”
Hata hivyo amewataka wakuu wa wilaya za Dodoma kuitumia taasisi hiyo ili kupata mifumo mbalimbali itayo wasaidia kujibu kero mbalimbali katika maeneo yao.
Meneja Masoko kampuni ya DIT, Agnes Kimwaga,amesema kuwa Taasisi hiyo imeaanza kubiasharailisha bunifu mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na wanafunzi wake ili kwenda kujibu changamoto zilizopo katika jamii.
“Kampuni hii itaweza kuuza bunifu zote ambazo zimefanywa kwa kuzipeleka sokoni na kuziuza badala ya kubaki katika makabati bila kuwa na tija”amesema Kimwaga
Aidha amesema kuwa kabla ya kuanzishwa kampuni hiyo tanzu bunifu nyingi zilikuwa zinabaki na kufungiwa kwenye makabati ofisini bili kuwa na manufaa kwa taasisi na jamii.
“Tumekuwa tukiandaa bunifu mbalimbali kupitia wanafunzi wetu lakini zinaishia kwenye makabati sasa tumeamua kuzibiasharailisha bunifu zote ili kwenda kujibu changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii”amefafanua Kimwaga
Hata hivyo Kimwaga amemshukuru Mtaka kwa kuwa tayari kufanya kazi pamoja na DIT
“Tunamshukuru Sana Mhe.Mtaka kwa kuwa tayari kufanya kazi pamoja na sisi na kesho tunaanza na hiyo ya bodaboda ambayo imetengenezwa na Dkt.Budoya
“Na kikubwa zaidi tumekaribishwa kila wilaya na sisi tutaenda kila wilaya ambazo tumekaribishwa na tutafika pia mpaka ngazi ya kata na tutakuwa tumefanya kazi kubwa”.Amesema Kimwaga
No comments:
Post a Comment