Watumishi TIC watoa msaada Kwa wagonjwa wa Saratani Hospitali ya Ocean Road. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 24, 2022

Watumishi TIC watoa msaada Kwa wagonjwa wa Saratani Hospitali ya Ocean Road.

Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wawekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bi. Anna Lyimo (kushoto) akimkabidhi baadhi ya vifaa Matroni wa wagonjwa wa saratani katika Hospitali Ocean Road, Chausiku Chapuchapu (kulia) leo Juni 24,2022 jijini Dar-es-salaam


Na Mwandishi wetu-Dar es Saalam. 

Katika kuendeleza utamaduni wa kujitoa kwa Jamii, Watumishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), wametoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wagonjwa wa Saratani waliolazwa Hospitali ya Ocean Road.

Vifaa vilivyotolewa kwa wagonjwa hao ni pamoja na miswaki, dawa za meno, mafuta ya kupaka, sabuni, kanga, madera, maji ya kunywa vitakavyo wasaidia wakati wakiendelea kupatiwa matibabu.

Akizungumza baada ya kutembelea na kutoa msaada huo kwenye Hospitali hiyo, Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wawekezaji Bi. Anna Lyimo akimuwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa (TIC), amesema taasisi hiyo, huo utakuwa ni utaratibu wake kuendelea kushirikiana nao kwakuwa wanafahamu mahitaji yao.

“Tangu Juni 16, 2022 tulianza kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma na tumehitimisha leo Juni 24, 2022 kwa kuwatembelea wagonjwa wa saratani kuja kuwaona na kuwaletea msaada wa vifaa ambavyo vitakuwa vinawasaidia.

"Tumepokea wananchi pamoja na wadau wa uwekezaji zaidi ya 70 kwenye ofisi zetu na kuwapa elimu juu ya fursa za uwekezaji na tumehitimisha kwa kuja kutoa msaada kwa wagonjwa waliopo mahali hapa” amesema Bi.Anna

Matroni wa wagonjwa wa saratani katika Hospitali hiyo, Chausiku Chapuchapu ameshukuru baada ya kupokea msaada huo huku akieleza kuwa wapo wagonjwa waliolazwa ambao ndugu zao wako mbali hivyo utawasaidia.

“Wagonjwa wetu wanashukuru kwa misaada wanayopokea kutoka kwa taasisi na watu mbalimbali kwakuwa waliowengi ndugu zao wako mikoani ”, amesema Chapuchapu

Hata hivyo Watumishi wa TIC akiwemo Afisa Uwekezaji Bi. Veronica Mrema amesema wamepata faraja kusaidia wagonjwa wa saratani na wameahidi kurudi wakati mwingine.

No comments:

Post a Comment