MKANDARASI JENGO LA WIZARA ATAKIWA KUWEKA KALENDA YA UJENZI ILI LIKAMILIKE KWA WAKATI.  - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 16, 2022

MKANDARASI JENGO LA WIZARA ATAKIWA KUWEKA KALENDA YA UJENZI ILI LIKAMILIKE KWA WAKATI. 



Na WMJJWM, Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ametoa siku tatu kwa Mhandasi wa Jengo jipya la Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma kuwa ameweka mtiririko na hatua za ujenzi hadi kukamilika kwa jengo hilo.


Dkt. Gwajima ametoa agizo hilo  Julai 13, 2022 mara baada ya kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Jengo hilo lililopangwa kukamilika ndani ya miezi 24 ya kazı.

Waziri Dkt. Gwajima amesema jengo hilo la Ghorofa Nane, litagharimu Bil. 29.9 hadi kukamilika kwake hivyo Kasi ya ujenzi iongezeke ili kuendeleza kasi ya utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Nimefika hapa nikiwa na Naibu Waziri wangu Mwanaidi Ali Khamis (Mb) kwa lengo la kukagua hali ya ujenzi ambapo tumemkuta Mkandarasi anaendelea lakini kubwa baada ya ukaguzi nimeagiza Mkandarasi kuandaa Kalenda ya Ujenzi ambayo ndio itakuwa 'Road Map' kujua kama kazi inakwenda kwa Kasi stahiki au la" amesema Dkt. Gwajima.

Aidha Waziri Dkt. Gwajima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kuanzisha Wizara na kuwapatia eneo la kujenga Ofisi ya Wizara.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maendeleo Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amesema atasimama imara miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa jengo hilo na endapo atabaini kuwepo kwa mapungufu au ucheleweshaji wa Mradi husika hatosita kuchukua hatua stahiki.

Akitoa taarifa ya ujenzi mbele ya Viongozi hao, Mkandarasi wa Jengo hilo la Wizara Michael Mussa amesema maelekezo yote ya Wizara yatatekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi. 

"Nitahakikisha nakamilisha kazi hii kwa wakati na kwa viwango vilivyokubalika" alisema.

Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ulianza rasmi tarehe 23 Juni, 2022 chini ya Mshauri elekezi, Wakala wa Majengo Nchini TBA

No comments:

Post a Comment