![]() |
| Mkurugenzi wa Fedha na Utawala ( PSPTB) CPA Paul Bilabaye akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea Banda la PSPTB. |
BODI ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB),inawakaribisha wanafunzi na wadau mbalimbali kutembelea banda la bodi hiyo ili kupata elimu ya namna ya kujisajili kupitia njia ya mtandao.
Akizungumza Julai 7,2022 katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yanayaofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Meneja Masoko na Uhusiano wa Umma kutoka Bodi hiyo Shamim Mdee amesema kuwa wapo katika Maonesho hayo ndani ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango.
Shamim ameeleza kuwa kwa sasa usajili haufanyiki ofisini bali unafanyika kwa njia ya mtandao hivyo waombaji wamekuwa wakisema kuna changamoto za kujisajili kwa njia hiyo ya mtandao.
" Waje hapa tuwapatie elimu ya kujisajili kwa njia ya mtandao kupitia simu zao za mkononi, Kompyuta mpakato na Desktop au jinsi ya kujisajili katika mitihani ya bodi kwa mwanachama wa bodi," ameeleza Shamim.
Aidha ameongeza kuwa wadau hao watembelee banda hilo na kutoa mrejesho kuhusiana na huduma wanazozipata ili serikali ipate kufahamu kinachoendelea kupitia bodi hiyo.
Meneja Masoko huyo amesema kuna wanachama mbalimbali wanahama taasisi moja kwenda nyingine halafu Bodi hiyo haifahamu hivyo ni vema kupitia maonesho hayo wakatembelea banda hilo ili kupata taarifa zaidi.
"Hii ni fursa nzuri kwao za kuja katika banda hili na kuweza kuhuishi taarifa zao, ameeleza Meneja Masoko huyo.


No comments:
Post a Comment