
- -
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Cheo kipya cha Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP) aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camillus Mwongoso Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Julai, 2022 |
 |
Balozi Dkt. Suleiman Haji Suleiman kushoto, Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule, Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Simon Nyakoro Sirro na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camillus Mwongoso Wambura wakila kiapo cha maadili ya Uongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa rasmi na Mhe. Rais Samia Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Julai, 2022 |
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi Camillus Mwongoso Wambura mara baada ya kumwapisha kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Julai, 2022 |
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na CP Mussa Ali Mussa kushoto, Kamishna wa Fedha na Lojistik CP Liberati Sabas Materu, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi CP Awadhi Juma Haji, na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad katika Hafla ya kumwapisha (IGP) Camillus Mwongoso Wambura Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Julai, 2022 |
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi Camillus Mwongoso Wambura na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Nyakoro Sirro mara baada ya kumwapisha (IGP) Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Julai, 2022 |
Na Okuly Julius-Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan leo Julai 20,2022 amewaapisha viongozi wapya wanne aliowateua na kuwataka kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na mahusiano mema na raia.
Akizungumza katika mara baada ya hafla ya uapisho uliofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma Rais Samia amesema ni muhimu kufanya kazi kwa ufanisi na kujenga mahusiano mema na raia.
Kuhusu suala la jeshi la Polisi nchini Rais Samia amesema linatakiwa kujitazama upya ambapo tayari ameshaunda kamati ya watu 12 kwa ajili ya kumshauri kwenye utendaji bora wa haki jinai
Katika hatua nyingine Rais Samia amesema idara ya Habari,Maelezo inatakuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha mifumo ya utendaji kazi ndani ya jeshi la polisi inaimarika.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Hamad Masauni ametumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wapya walioteuliwa.
Viongozi wapya walioteuliwa na kuapishwa ni pamoja na aliyepandishwa cheo kamishna wa polisi Camillus Wambura aliyekuwa mpelelezi wa makosa ya jinai [DCI] kuwa Inspekta Jenerali na mkuu wa jeshi la polisi,aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi Simon Sirro kuwa balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe,amempangia kituo Balozi Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia na mwingine ni Dkt.Suleiman Haji Suleiman kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa afisa Wizara ya mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment