![]() |
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, ADAM FIMBO akizungumza jijini Dodoma na waandishi wa habari leo Julai 28,2022 wakati akielezea mafanikio ya Mamlaka hiyo kwa mwaka 2021/22 na matarajio kwa mwaka 2022/23 . |
Na Okuly Julius-Dodoma
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA, imekamata aina mbalimbali za dawa zikiwemo za serikali, vifaa tiba na vitendanishi ambavyo hazijasajiliwa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 350 katika operesheni maalum iliyofanyika katika mikoa 14 hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, ADAM FIMBO akizungumza jijini Dodoma na waandishi wa habari leo Julai 28,2022 wakati akielezea mafanikio ya Mamlaka hiyo kwa mwaka 2021/22 na matarajio kwa mwaka 2022/23 .
Ambapo Bw.Fimbo amesema kuwa operesheni hizo tatu zilizofanyika kwenye maeneo 1,355 ya biashara zimewezesha kukamatwa kwa aina 4 za dawa bandia, aina tano za dawa duni dawa za serikali na dawa ambazo hazijasajiliwa, huku thamani ya dawa na vifaa tiba vya serikali ikifikia shilingi milioni 13.
Bw.Fimbo amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2021/2022 mamlaka hiyo imesajili jumla ya maeneo 467 yanayojihusisha na biashara za bidhaa zinazodhibitiwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa maeneo husika yanakidhi vigezo ili kutoathiri ubora,ufanisi na ufanisi wa bidhaa.
"Jumla ya maeneo 10,938 yanayohusisha na biashara ya dawa,chanjo,vifaa tiba na vitendanishi yalikaguliwa kwa mwaka 2021/22 ikiwa ni ongezeko la maneno 92 yaliyokaguliwa ikilinganishwana maeneo 10,846 yaliyokaguliwa mwaka 2020/2" Amesema Fimbo
Akielezea mpango mkakati wa kitaifa wa miaka mitano 2021 hadi 2026 wa kupambana na tumbaku pamoja na mpango kazi wa miaka mitano wa udhibiti wa tumbaku, mkurugenzi mkuu huyo wa TMDA amesema mfumo wa udhibiti wa bidhaa hizo na hadi sasa wamekwisha tambua bidhaa zote za tumbaku zilizoko kwenye soko ambapo idadi yake ni bidhaa 51.
Aidha,Mkurugenzi mkuu huyo amesema kuwa kwa sasa mamlaka hiyo imeanzisha maabara ya upimaji wa bidhaa za tumbaku kwenye jengo lake lililoko jijini Dodoma.
Kuhusu ukaguzi wa Viwanda 15 vya dawa (8 vilivyosajiliwa na 7 vipya) ndani ya nchi vilikaguliwa ambapo viwanda viwili (2) kati ya 7 vipya vimekidhi vigezo na vinatarajiwa kuanza uzalishaji hivi karibuni. Hili Ni ongezeko la viwanda 6 sawa na 67% ikilinganishwa na viwanda 9 vilivyokaguliwa mwaka 2020/21.
Aidha, jumla ya viwanda vipya 21 vya vifaa tiba vilisajiliwa ikiwa ni ongezeko la viwanda 18 ikilinganishwa na viwanda vitatu (3) vilivyosajiliwa mwaka 2020/21. Hadi kufikia mwezi Juni 2022 jumla ya viwanda 17 vya dawa, 26 vya vifaa tiba na 6 gesi tiba vimesajiliwa na kuanza kufanya kazi.
Moja ya majukumu ya TMDA ni pamoja na kusajili bidhaa za dawa,vifaa tiba na vitendanishi, katika kipindi cha mwaka 2021/2022, mamlaka hiyo imesajili jumla ya bidhaa 1,286 ambapo kati yake bidhaa za dawa za binadamu na mifugo ni 933 huku vifaa tiba na vitendanishi vikiwa ni 353 na hivyo kufanya idadi ya bidhaa zilizosajiliwa kufikia 8,831 hadi sasa.
No comments:
Post a Comment