Na Okuly Julius-Dodoma
Mhe Simbachawene ameyasema hayo leo Julai 29,2022 jijini Dodoma wakati akielezea vipaumbele vya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera ,Bunge na Uratibu) na taasisi zilizochini yake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na kusema kuwa Ongezeko hilo la bajeti ya mamlaka hiyo litaendelea kuimarisha udhibiti wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini, kuimarisha ushirikiano miongoni mwa Vyombo vinavyojihusisha na udhibiti wa Dawa za Kulevya kitaifa na kimataifa.
Aidha, Simbachawene amesema kuwa fedha hizo zitatumika katika kubadilishana taarifa na kuimarisha ukusanyaji wa taarifa za kiintelijensia zinazohusu biashara haramu ya Dawa za Kulevya na kuendesha operesheni za pamoja.
"Ofisi itaboresha huduma za tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya kwa kuongeza idadi ya vituo vya tiba na urekebishaji wa tabia ya waathirika wa Dawa za Kulevya nchini"Amesema Simbachawene
Na kuongeza kuwa "pamoja na kuweka programu maalum ya elimu ya maisha (Life skills) na mafunzo ya ufundi pamoja na kuwapatia vifaa (startup kits) ili waweze kuajiriwa au kujiajiri na hivyo kuwa na shughuli za kiuchumi za kufanya"Amesema
Mhe.Simbachawene amesema Kwa upande wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania imeidhinishiwa na Bunge zaidi ya Shilingi bilioni 14.9 ambapo zaidi ya shilingi bilioni 2.9 ni kwa ajili ya matumizi ya Kawaida na Shilingi bilioni 12.0 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ukiilinganisha na bajeti ya Shilingi bilioni 3.17 zilizotengwa mwaka 2021/22 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za matumizi ya kawaida na maendeleo sawa na ongezeko la asilimia 71.2.
Amesema kuwa shughuli zitakazotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/23 ni pamoja na kuratibu upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI kwenye Mikoa ya kipaumbele ikiwemo; Iringa, Kagera, Katavi, Mbeya, Mwanza, Njombe, Pwani, Ruvuma, Shinyanga, Dodoma, Geita, Tabora na Songwe pamoja na kuweka kipaumbele katika kuzuia maambukizi ya VVU kwa vijana wa miaka 15 - 24.
No comments:
Post a Comment