KOMESHENI AJIRA ZA WATOTO MIGODINI-DKT.MPANGO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 12, 2022

KOMESHENI AJIRA ZA WATOTO MIGODINI-DKT.MPANGO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akizungumza leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO
Waziri wa Madini Dkt Dotto Biteko akizungumza leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Selemani Jafo akizungumza leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO Dkt.Venance Mwasse akizungumza leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akizungumza leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango (kulia) pqmoja na Waziri wa Madini Dkt Dotto Biteko wakijitaharisha kuzindua Mkaa Mbadala utakaotumika na wananchi ambao utapunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazizingira tukio hilo limekwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango (kulia) pqmoja na Waziri wa Madini Dkt Dotto Biteko wakizindua Mkaa Mbadala utakaotumika na wananchi ambao utapunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazizingira tukio hilo limekwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.


Na Okuly Julius-Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha ajira za watoto migodini zinakomeshwa.

Ameyabainisha hayo leo Agosti 12,2022 Jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambapo amezitaka Wizara ya Madini, STAMICO na NEMC kuongeza kasi ya ukaguzi katika migodi ili kubaini na kudhibiti uharibifu wa mazingira.

"Bado kuna migodi haizingatii utunzaji wa mazingira wanaachia maji machafu yenye madini ya Zebaki kuingia kwenye vyanzo vya maji hivyo kuleta madhara kwa wananchi niwatake wizara husika ,STAMICO na NEMC kudhibiti jambo hili haraka kabla halijaleta matatizo makubwa"Amesema Dkt.Mpango

Aidha,Dkt Mpango ameitaka wizara ya Madini kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kuhakikisha wanaweka mazingira rafiki ya afya kwa wachimbaji wa madini na kuboresha vitendea kazi ili visilete madhara kwa wachimbaji.

Akijibu changamoto zilizowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO Dkt.Mpango amesema kuwa Mhe.Rais Samia amezipokea na kuahidi kuwa atashughulikia changamoto hizo za upatikanaji wa ajira pamoja na kuboresha biashara ya manunuzi ya umma.

Naye Waziri wa Madini Dkt Dotto Biteko amesema licha ya Shirika hilo kufanya vizuri katika soko la ndani lakini amelitaka kuhamishia nguvu katika biashara kiushindani kimataifa.

Pia Biteko amesema kuwa mageuzi makubwa yaliyofanyika ndani ya shirika hilo ndio yameleta mafanikiao ambapo zaidi ya ajira 700 zimezalishwa ndani ya mgodi wa Kiwira.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Selemani Jafo ameitaka STAMICO kuongeza uzalishaji wa Mkaa mbadala na kusambaza kwa wananchi ili kutunza mazingira huku akizitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa STAMICO katika utunzaji wa mazingira.

Akizungumza Mafanikio ya Shirika hilo Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO Dkt.Venance Mwasse amesema shirika limefanikiwa kufufua mgodi wa Kiwira ambao ulikufa toka mwaka 2012 ambapo kwa sasa unaendelea nashughuli zake kama kawaida pamoja na kusaini mkataba wa kuuza makaa ya mawe elfu sitini yenye thamani ya shilingi bilioni nne.

Dkt.Mwasse amesema licha ya kuwepo kwa mafanikio makubwa katika shirika hilo lakini bado zipo changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa wafanyakazi, taratibu za ununuzi wa umma bado sio rafiki kwa biashara.

Naye mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kuwa Mkoa wa Dodoma una Madini mengi sana hivyo amewaomba Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika kuhadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake wasaidie kutambua kiasi cha madani yaliyopo katika mkoa wa Dodoma

"Niwaombe STAMICO Dodoma ni mkoa ambao una madini mengi sana hivyo tunahitaji kujua ni kiasi gani ya madini tulionayo katika mkoa wetu kwani tumekuwa tukifanya tu makisio naamini Dodoma ina madini aina nyingi nafikiri kasoro tu madini ya Tanzanite"Amesema Senyamule

Shirika la Madini la Taifa STAMICO limesherekea miaka yake 50 tangu kuanzishwa kwake kwa kutoa gawio la shilingi bilioni 2.2 kwa serikali ikiwa ni sehemu ya faida yake.

No comments:

Post a Comment