Na Okuly Julius-Dodoma
Ameyasema hayo leo Agosti 6,2022 jijini Dodoma Mbele ya waandishi wa habari wakati akitoka taarifa ya shirika hilo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya shirika 2021/22 na mikakati Kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Kadogoso amesema katika kuboresha miundombinu Serikali inajenga mfumo wa umeme wa msongo wa kilovoti 220 ambao unajitegemea kwa ajili ya uendeshaji wa treni ili kupata umeme wa uhakika,Kwa kipande Cha Dar es salaam mpaka Morogoro mfumo huo una urefu wa kilimeta 160 na umekamilika Kwa asilimia100,mkandarasi ameshalipwa kiasi Cha bilioni 70.6.
"Mpaka sasa tupo vizuri ambapo kipande cha Morogoro mpaka makutupora ujenzi wa msongo wa kilovoti 220 ambao unaendelea na una jumla ya kilimeta 410 na mkataba wake ni shilingi bilioni 160.2, mpaka sasa Wakandarasi wamelipwa shilingi bilioni 29.4 na bilioni 48.5 Kila Moja" Amesema Kadogoso
Amesema pamoja na kuwa na majukumu mengine pia shirika hilo kwa mwaka wa fedha 2021/22_2022/23 limejikita zaidi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi ya shirika Kwa kujenga,kukarabati na kuboreshwa miundombinu ya Reli ununizi wa ukarabati na vitendea kazi .
Kadogosa amesema ili kufikia adhma hiyo shirika litahakikisha linaboresha miundombinu ya Reli Kwa kujenga mtandao mpya wa Reli wa kiwango Cha standard Gauge wenye jumla kilimeta 4,777 na ukarabati wa mtandao wa Reli iliyopo ya Meter Gauge Kwa kilimeta 2537.
Aidha, amesema kuwa ukarabati huo wa njia ambao utajumuisha kuinua uwezo wa njia Kwa kuondoa reli nyepesi za paundi 45 na 56 na kutandika Reli nzito za paundi 80,kuinua uwezo wa madaraja kutoka ekseli 13.5 kufikia ekseli 18.5 pamoja na kuboreshwa mfumo wa ishara na mawasiliano.
Pia amezungumzia upande wa miradi mingine na kusema kuwa shirika hilo linatekeleza miradi ya muda mfupi, muda wa kati na mrefu ,pia muda mfupi inajumuisha miradi ufufuaji wa njia za zamani ikiwemo njia ya kaskazini ,miradi ya muda wa kati inajumuisha ukarabati wa njia iliyopo ikiwemo uboreshaji wa njia ya kati ambao umefanyika kupitia Mradi wa Tanzania Intermodal and tall Development project (TIRP) kutoka Dar es salaam hadi Isaka, Miradi ya muda mrefu ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR).
Kwa Upande wake Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alisema ujenzi wa reli hiyo unaenda sambamba na Maboresho ya bandari zilizopo nchini kwa kuwa miundombinu hiyo ni mahsusi kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo mizito.
No comments:
Post a Comment