Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Khamis Abdulla kwa mara ya kwanza leo tarehe 30 Agosti, 2022, amefanya ziara yake katika katika Ofisi Kuu za Shirika la Posta Tanzania, mjini Zanzibar.
Lengo la ziara yake ni kujionea namna Shirika la Posta linavyofanya shughuli zake katika kuwahudumia wananchi hususani katika eneo la usafirishaji wa barua, nyaraka, mizigo na vipeto, mjini humo
Aidha, Bw. Mohamed Abdulla ametumia nafasi hiyo kulitaka Shirika la Posta Tanzania kuendelea kuboresha mifumo yake ili kurahisisha utendaji kazi utakaowezesha kuendelea kutoa huduma zenye ubora kwa wananchi
Sambamba na hilo, Naibu Katibu Mkuu amelipongeza Shirika la Posta kwa jitihada zake mbalimbali za kuendelea kuboresha huduma zake ili kuendana na maendeleo ya Teknolojia Pamoja na mahitaji ya wananchi.
Ziara ya Naibu Katibu Mkuu ilienda sambamba na ukaguzi wa minara 42 itokanayo na mradi wa "Rural Telecommunication Border & Special Zone Phase 7 (BSZPH7)" iliyojengwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na kampuni ya Tigo-Zantel.
Ukaguzi huo ulifanywa na Naibu Katibu Bw. Mohamed Khamis Abdulla na Posta imeshiriki kama mdau wa Mawasiliano nchini aliyeshiriki ziara hiyo ni Meneja Mkaazi (TPC) Zanzibar Bw. Ahmad Mohammed Rashid
No comments:
Post a Comment