WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA WAHIMIZWA KUTUMIA VIZURI MISAADA INAYOTOLEWA NA WAHISANI KWA MANUFAA YA JAMII. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, August 27, 2022

WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA WAHIMIZWA KUTUMIA VIZURI MISAADA INAYOTOLEWA NA WAHISANI KWA MANUFAA YA JAMII.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Salum A. Manyatta akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kliniki ya Himophilia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya iliyoambatana na mafunzo kwa watoa huduma za afya wa Nyanda za Juu Kusini iliyofanyika Jijini Mbeya

Na Mwandishi wetu Mbeya 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Salum A. Manyatta amezindua rasmi Kliniki ya Himophilia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya hafla iliyoambatana na mafunzo kwa watoa huduma za afya wa Nyanda za Juu Kusini, matembezi ya hisani, uchunguzi wa wanaosadikika kuwa na ugonjwa wa hemophilia na zoezi la uchangiaji damu kwa lengo la kusogeza huduma za matibabu ya Hemofilia karibu na wananchi.

Akizindua Mradi huo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikari, Dkt. Manyatta amepongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Hosptali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kazi nzuri waliofanya hadi kukamilishia uanzishwaji wa Kliniki ya Himophilia pamoja na kuwaelekeza watumishi wa Hospitali kutumia vizuri msaada unaopokelewa kwa manufaa ya Mkoa, Kanda na Jamii kwa ujumla.

“Sambamba na pongezi hizi, ningependa kutoa maelekezo yafuatayo, watumishi wa hospitali kutumia vizuri msaada unaopokelewa katika Hospitali hii kwa manufaa ya Mkoa, Kanda na jamii yetu kwa ujumla, pia watumishi waliopokea elimu ya himofilia kuendeleza na kufikisha elimu hiyo kwa watu wengi zaidi katika hospitali zao husika”- Dkt. Manyatta.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasio ambukizwa kutoka wizara ya afya Dkt. James Kiologwe  amesema lengo kuu la mradi ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya katika kupunguza madhara ya vifo vinayotokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Himophilia pamoja na kuwezesha upatikaji wa vipimo vya magonjwa ya damu ikiwemo (Selimundo na Himophilia), mafunzo na upatikanaji wa wataalamu waliobobea katika hospitali za rufaa nchini.

Dkt. Kiologwe ameeleza kuwa utume wa Wizara ya Afya ni kuhakikisha inaboresha afya kwa wananchi kwa kuwawezesha kuwa na afya bora ili aweze kushiriki kujiletea maendeleo na maendeleo kwa taifa na katika kusimamia utumie wa Wizara, kupitia mradi huu wa Hemophilia Wizara itaendelea kushirikiana na wadau kutengeneza mikakakati ya huduma endelevu na jumuishi nchini Tanzania.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru, amewashukuru wafadhili wa mradi huu Novo Nodisk Haemophilia Foundation, Novo Nodisk Foundation, Wizara ya Afya na wasimamizi wa mradi kwa msaada mkubwa waliotoa kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Hospitali nyingine nchini ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya katika jitihada za kuwezesha uboreshaji wa huduma za wagonjwa wa Himophilia na Selimundo nchini. 

Dkt. Godlove Mbwanji, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jinsi walivyotimiza wajibu wao katika kusaidia kuanzisha huduma hizi ambazo zitawapunguzia wananchi mzigo mkubwa wa kusafiri umbali mrefu wa kwenda kupata matibabu Dar Es Salaam na kutoa wito kwa taasisi, mashirika na watu mbali mbali kutoa michango yao kwa hospitali nchini ili kuwasaidia wananchi wasio kuwa na uwezo wa kumudu gharama za matibabu . 

Himophilia ni Ugonjwa wa damu wa kurithi unaotokana na upungufu wa chembechebe au protini zinazo saidia damu kuganda, kwa hiyo mtu anapopata jeraha au hata asipopata jeraha damu hutoka kwa muda mrefu bila kuacha ambapo kati ya watu 10000 mtu mmoja anakuwa na ugonjwa huo ambapo kwa takwimu za Tanzania na takrabani kati ya watu Mil. 60 watu Mil .6 wana ugonjwa wa Himophilia na kwa wagonjwa wanaotambuka tayari ni wagonjwa 190.

No comments:

Post a Comment