NAKUOMBA UWEKE UZITO MKUBWA KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI JIJINI DODOMA-SENYAMULE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 16, 2022

NAKUOMBA UWEKE UZITO MKUBWA KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI JIJINI DODOMA-SENYAMULE


Na Okuly Julius-Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amemuomba waziri wa maji Mheshimiwa Jumaa Aweso kuweka uzito wa kutosha katika kutatua changamoto ya maji katika Jiji hilo kutokana na ongezeko la watu wanaohamia kwa kutekeleza maelekezo ya serikali.

Akizungumza leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa programu ya maendeleo ya sekta ya maji awamu ya tatu Senyamule amesema kuwa Mkoa wa Dodoma bado una changamoto ya maji kwa baadhi ya maeneo huku maeneo ya vijijini ikiwa na asilimia 65.1 ya maji na mjini ni asilimia 57.

Senyamule amesema kuwa Mkoa wa Dodoma ni fahari ya Watanzania hivyo ili iwe fahari kweli kweli haipaswi kuwa na changamoto ya maji.

"Hatuwezi kuwa fahari ya watanzania wakati kuna baadhi ya maeneo hayana huduma ya maji na ili tuwe fahari nikuombe Mheshimiwa Aweso na najua hili unaliweza weka uzito mkubwa katika awamu hii ya tatu kwa Dodoma hii ambapo kila siku tunapokea wageni wengi ambao wanakuwa wakaazi na wanahitaji maji,"Amesema Senyamule


No comments:

Post a Comment