Na Okuly Julius-Dodoma
Majadiliano hayo yatatokana na hatua iliyofikiwa katika mapitio ya Sera na mitaala baada ya kukusanya maoni mengi kutoka kwa wadau kupitia mikutano mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 25,2022 jijini Dodoma Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa Mkutano huo utaanza Septemba 26 mpaka 28,2022 jijini Dodoma.
Prof.Mkenda amesema kuwa Mkutano huo unajumuisha wahadhiri,waajiri,wadau wa maendeleo,taasisi za umma na binafsi,taasisi za dini,taasisi zisizo za Kiserikali,taasisi zinaohusika na uendeshaji wa lugha,Jumuiya za kitaaluma,Taasisi za Sayansi na Utafiti na timu ya Zanzibar inayopitia Sera na mitaala ikiongozwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.
Katika hatua nyingine, Waziri Prof Mkenda amesema kuwa tarehe 27 Septemba, 2022 serikali itafungua rasmi dirisha la maombi ya ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIPS”.
"Mtakumbuka Wizara yetu ilitoa ahadi kupitia hotuba ya bajeti ya kuanzisha programu mpya ya kutoa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa wahitimu bora wa kidato cha sita katika masomo ya sayansi. Siku hiyo tutatangaza rasmi Mfumo wa uombaji na vigezo" Amesema Prof.Mkenda
Pia Prof.Mkenda ameukumbusha umma kuwa serikali imezindua tuzo za waandishi bunifu zijulikanazo kama Tuzo za Mwalimu Nyerere, hivyo ameendelea kukaribisha Waandishi Bunifu wa Riwaya na Mashairi kuwasilisha maandiko yao ili kuwania tuzo hizo.
Prof Mkenda amesema kuwa Mwisho wa kupokea Mawasilisho hayo ni Novemba 30, 2022 ambapo kwa taarifa zaidi kuhusu tuzo hizo na maulizo wanaweza kufuatilia katika akaunti maalumu za mitandao ya kijamii za tuzo Nyerere au mitandao na tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Taasisi ya Elimu Tanzania-TET kwa anuani ya tuzonyerere@tie.go.tz
No comments:
Post a Comment