MAONI YA KUBORESHA NI MUHIMU SANA -PROF.MKENDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, September 26, 2022

MAONI YA KUBORESHA NI MUHIMU SANA -PROF.MKENDA

Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akizungumza leo Septemba 26,2022 jijini Dodoma wakati akifungua kikao maalumu cha Menejiment ya wizara na wadau wa elimu kitakachofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 26 mpaka 28,2022 jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Ali Abdugulam Hussein akizungumza leo Septemba 26,2022 jijini Dodoma wakati wa kikao maalumu cha Menejiment ya wizara ya elimu na wadau wa elimu kitakachofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 26 mpaka 28,2022 jijini Dodoma
Sehemu ya washiriki wa kikao maalum cha Menejiment ya Wizara ya Elimu na wadau wa elimu kitakachofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 26 mpaka 28,2022 jijini Dodoma

Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amewataka wadau wa elimu nchini wanaoshiriki katika kikao maalum cha Menejiment ya wizara na wadau wa elimu kutoa maoni ya kuboresha sera na mitaala ya Elimu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sekta hiyo muhimu Duniani.


Akizungumza leo jijini Dodoma Prof . Mkenda amesema kuwa kikao hicho ni kutekeleza Agizo la Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania samia suluhu hassani ambapo Mnamo Tarehe 22 April 2022 Bungeni alisema kufanyike marekebisho ya sera ya Elimu ya mwaka 2014 pamoja na mitaala iliyopo kwa maslahi ya Taifa na Watu wake.

Prof.Mkenda amesema kuwa huwezi kuzungumzia ubora wa elimu bila kufanya mageuzi na mabadiliko katika sera na mitaala ili kuendana na kasi ya maendeleo ya Dunia kwani kwa sasa taaluma na ujuzi zinakwenda sambamba.

"Tunapokwenda kufanya mageuzi ya elimu ni lazima twende na adhma ya Mhe.Rais aliyeagiza kuwa mbali tu na kujikita katika elimu ya taaluma tujikite pia katika Ujuzi hivyo ni lazima tuhakikishe tunatoa mawazo ambayo itasaidia kuboresha elimu yetu sio kushusha ubora,"Amesema Prof.Mkenda

Na kuongeza kuwa "Swala la elimu sio la Tanzania peke yake ni la kidunia hivyo lazima tufanye mageuzi ili kuendani na kasi ya mabadiliko katika sekta ya elimu duniani,"Amesema


Kwa upande wake naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Abdugulam Hussein amesema vijana lazima waandaliwe kitalamu na kiubunifu ili waweze kulitetea Taifa kimaendeleo na kushindana kimasoko.

Pia Mhe. Ali Abdugulam Hussein amesema kuwa swala la sera na mitaala ya elimu ndio kila kitu katika maboresho ya elimu hivyo kukifanyika makosa katika mapitiao haya yanaweza kulipoteza taifa.

"Sera na mitaala ni vyanzo muhimu katika elimu ya nchi yeyote duniani hivyo niwaombe washiriki wa kikao hiki maalum mtoe mawazo huku mkijua kuwa michango yenu ndio itakayokuja na sera na mitaala madhubuti,"Amesema Mhe. Ali Abdugulam Hussein

Dhima ya sera mpya na mitaala ya Elimu nchini ni kuinua ubora wa Elimu na Mafunzo na Kuweka Mifumo na Taratibu Zitakazowezesha Kupata idadi Kubwa ya Watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikisha Malengo ya Maendeleo ya Taifa.

No comments:

Post a Comment