Na Okuly Julius-Dodoma
Ameutoa ushauri huo wakati akifungua mkutano wa kitaifa wa majadiliano juu elimu jumuishi uliondaliwa na Shirika la Child Support Tanzania kupitia mradi wa peleka rafiki zangu wote shule Septemba 2,2022 Jijini Dodoma.
Spika Ackson amesema kupitia mkutano huo wanatakiwa kujadiliana namna bora ya kuisaidia elimu jumuishi Tanzania kwani kuna baadhi ya maeneo hayajakaa vizuri.
“Mawazo mtakayatoa kuhusu elimu yetu yatawekewa uzito kwenye elimu jumuishi maana yake ile mitaala inapoboreshwa itakuwa inatizama pia katika elimu jumuishi wapi hatujafanya vizuri kama Taifa,"Amesema Dkt.Tulia
Na kuongeza kuwa “Mkutano huu ni wa muhimu kwa sababu Nchi ipo katika mchakato huo utatoa maoni mazuri ili usiche mtu wowte.Mkipata fursa ya kujadili hili jambo litatisaidia kama Bunge namna ya kuishauri Serikali ili ifanye vizuri zaidi,”
Aidha Spika Tulia amesema watoto wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa miundombinu,ukosefu wa vifaa visaidizi vya kuwasaidia, pamoja na kukosekana kwa uratibu wa kugharamia elimu jumuishi kwa sababu mahitaji yao ni maalum zaidi ya watoto wa kawaida.
“Upimaji wa watoto wenye ulemavu nao ni lazima uangaliwe kwani wapo tofautitofauti.Shule chache zina pima ulemavu wa watoto hili ni lazima liangaliwe kwani ulemavu unatofautiana,”amesema.
Ameongeza kuwa inatakiwa kufika wakati mtoto mwenye ulemavu wasione wameachwa nyuma na anaamini mambo hayo yataenda vizuri ili waone namna bora ya kuishauri Serikali.
Vilevile,Spika Tulia ameishauri Serikali kutowasahau watoto wenye ulemavu ikiwemo kwenye suala la madawati kwani wao ni kama wamesahaulika.
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Child Support Tanzania,Noelah Msuya amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata elimu huku akidai tayari wamishawafikia wanafunzi 1000 katika shule 51 mkoani Mbeya,Rukwa na Dodoma.
Amesema bado watoto wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto za uhaba wa walimu wa elimu jumuishi na jamii haina uelewa kuhusu elimu jumuishi pamoja na haki na usalama wa watoto.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa Child Support Tanzania imebaini kuwa kumekuwa na changamoto katika jamii ambazo zimekuwa zikileta ugumu kwa watoto wenye ulemavu kushiriki katika elimu kutokana na sababu mbalimbali.
Ametaja moja ya sababu inayopelekea baadhi ya wazazi kushindwa kuwapelekea watoto wenye ulemevu mashuleni kuwa wengi wanahofia usalama wa watoto hao pamoja na wengine kuona kuwa na mtoto mlemavu ni mkosi au laana jambo ambalo linapelekea kuwafungia ndani muda wote.
"Kikweli tunaakutana na changamoto ila wakati mwingine kuna sababu za msingi kabìsa za wazazi hao kuwazuia watoto wenye ulemavu na kuwafungia ndani wengine ni kwa sababu ya usalama wao kwa sababu dunia imebadilika sana kwa sababu watu wanaweza kuwafanyia vitendo vya kikatili,"Amesema Msuya.
Mwenyekiti wa Viziwi na Wasioona Tanzania (TASODEB) David Shaba amemuomba Spika wa Bunge kulivalia njuga suala la watu wenye ulemavu kupata elimu pamoja na kutengwa bajeti maalum.
“Washawishi na wabunge wengine mambo yetu wasiyadharau, nashukuru kwa kutambua elimu maalum.Kuna umuhimu mkubwa wakuwa na elimu maalumu hatuwezi kutegemea ufadhili kutoka Nje wakati rasilimali zipo tunataka bajeti maalum kuhusu watu wenye ulemavu,”amesema Shaba
No comments:
Post a Comment