WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WATAKIWA KUSIMAMIA VIONGOZI WA ELIMU KATIKA NGAZI ZAO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 8, 2022

WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WATAKIWA KUSIMAMIA VIONGOZI WA ELIMU KATIKA NGAZI ZAO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa leo tarehe 8 Septemba, 2022 Jijini Dodoma akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa kwa umma ya uboreshaji wa huduma kwa walimu nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa leo tarehe 8 Septemba, 2022 Jijini Dodoma akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa kwa umma ya uboreshaji wa huduma kwa walimu nchini.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa leo tarehe 8 Septemba, 2022 Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa umma ya uboreshaji wa huduma kwa walimu nchini.

Na Okuly Julius-Dodoma

Serikali kupitia ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) imewataka Waakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kufatilia na kusimamia viongozi wa elimu katika ngazi ya Mikoa, Halmashauri, Kata na shule ili kutekeleza mikakati ya uboreshaji wa usimamizi wa Elimu Nchini ili kufanikisha malengo ya serikali ya kutoa elimu bora kwa mtoto wa kitanzania.

Akitoa taarifa kuhusu uboreshaji wa huduma kwa walimu Jijini Dodoma Waziri wa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa amesema ni Marufuku kuwaacha walimu kupita kila ofisi ya Halmashauri kutafuta huduma huku akisisitiza wasimamizi wanaotoa huduma kwa walimu kutimiza wajibu wao na kutokubweteka kukaa maofisini.

“Ni marufuku kuwaacha walimu kupita kila ofisi ya Halmashauri kutafuta huduma, narudia tena mwalimu apelekewe huduma shuleni badala ya watoa huduma kukaa ofisini” amesema Bashungwa

Amesisitiza kuwa Mwalimu akiandika barua kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhitaji huduma, anapaswa kujibiwa kwa maandishi ndani ya siku 7 baada ya kupokelewa.

Aidha, Bashungwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote nchini kuwasimamia Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Maafisaelimu, Maafisa wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Wathibiti Ubora wa Shule kuhakikisha wanawafuata walimu mashuleni na kutatua kero na malalamiko yao kwa wakati.

Amewataka viongozi hao kufuatilia na kuwasimamia viongozi wa elimu katika ngazi ya Mikoa, Halmashauri, Kata na shule kutekeleza mikakati ya uboreshaji na usimamizi wa elimu na kuhakikisha wanawasilisha taarifa ya utekelezaji Ofisi ya Rais – TAMISEMI kila robo mwaka.

Vile vile, amewataka kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Mafunzo kazini kwa walimu, kwa mujibu wa Mwongozo uliotolewa na Katibu Mkuu Utumishi na ufanyike kwa uwazi na ushirishwaji wa kutosha, ili kuondoa dhana ya kuwa waajiri wanatoa nafasi za mafunzo kwa upendeleo.

Pia, Bashungwa amewaelekeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwasimamia Maafisa wa Tume ya Utumishi wa Walimu kuzingatia miongozo ya upandishwaji vyeo walimu, ili kila anayestahili kupandishwa cheo, anapandishwa kwa mujibu Sheria, Kanuni na Miongozo.

Hata hivyo Katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zaidi ya walimu 157,923 (laki moja hamsini na saba elfu,mia tisa ishirini na tatu)wamepandishwa madaraja, wamerekebishiwa Muundo wa Utumishi na kulipwa mishahara kulingana na madaraja mapya, katika mwaka 2021 na 2022.

No comments:

Post a Comment