WAZIRI MKUU ATAKA KASI UJENZI BARABARA YA MZUNGUKO DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, September 4, 2022

WAZIRI MKUU ATAKA KASI UJENZI BARABARA YA MZUNGUKO DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Atupele Mwakibete wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3, Septemba 4, 2022. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama makaravati wakati alipokagua mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3 wakati alipokagua mendeleo ya ujenzi huo, Septemba 4, 2022. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule na wa tatu kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kaimu Meneja wa Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS ) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Salome Kabunda ( kushoto) ambaye alikuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3, Septemba 4, 2022. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3 ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake, Septemba 4, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Na Ofisi ya Waziri Mkuu 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakandarasi wa ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma kuongeza kasi ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati na kwa viwango.
 
 “Kazi inaendela vizuri, tunataka kazi ikamilike ikiwezekana hata kabla ya muda, Rais Samia Suluhu Hassan anatekeleza miradi hii ili iwanufaishe Watanzania, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunasimamia na inakamilika kwa viwango na wakati”
 
Amesema hayo leo (Jumapili, Septemba 04, 2022) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma. Mradi huo ni sehemu ya uendelezaji wa jiji hilo.
 
Pia, Waziri Mkuu amewataka Wahandisi Wasimamizi wa mradi huo wahakikishe wanasimamia kikamilifu wakandarasi ili barabara hiyo iweze kujengwa kwa viwango vilivyokubaliwa kwenye mkataba wa ujenzi wake.
 
Akizungumza na watanzania walioajiriwa katika mradi huo, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wawe walinzi wa vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi na wahakikishe vifaa vinabaki salama “Pambaneni na wote wenye nia ya kuiba vifaa hivi, tunataka tupate barabara yenye viwango”
 
Kaimu Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Salome Kabunda amesema kuwa pamoja na mradi huo kusaidia kupunguza msongamano wa magari jiji la Dodoma pindi utakapokamilika, pia umesaidia kutoa ajira kwa wazawa zaidi ya 800.
 
“Mheshimiwa Waziri Mkuu utekelezaji wa mradi huu utawezesha kujengwa kwa vituo vya afya vinne katika mitaa ya Mahomanyika, Veyula, Nala na Ihumwa. Pia yatanunuliwa magari ya wagonjwa manne katika vituo hivyo”.
 
Aliongeza kuwa sehemu ya kwanza ya ujenzi wa barabara hiyo kutoka Nala-Veyula-Mtumba hadi bandari kavu ya Ihumwa (Km 52.5) unaojengwa kwa muda wa miezi 39, utagharimu shilingi bilioni 100.

“Sehemu ya pili ya ujenzi wa barabara hii kutoka Bandari kavu ya Ihumwa-Matumbulu hadi Nala (Km 60) unaojengwa kwa muda wa miezi 43, utagharimu shilingi bilioni 120.8 ”

No comments:

Post a Comment