MATUMIZI HOLELA YA DAWA ZA MIFUGO KUSABABISHA VIFO VYA WATU MILIONI 10 KILA MWAKA IFIKAPO MWAKA 2030-TVLA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, October 21, 2022

MATUMIZI HOLELA YA DAWA ZA MIFUGO KUSABABISHA VIFO VYA WATU MILIONI 10 KILA MWAKA IFIKAPO MWAKA 2030-TVLA

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt.Stella Bitanyi ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 21,2022 jijini Dodoma.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt.Stella Bitanyi ,wakati akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 21,2022 jijini Dodoma.


Na Okuly Julius-Dodoma

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dk. Stella Bitanyi,ameeleza kuwa ifikapo mwaka 2030, watu zaidi ya milioni 10, watakufa kila mwaka kutokana na matumizi holela ya dawa za mifugo ambayo yamekuwa yakisabaishwa na vimelea vya magonjwa kujenga usugu.

Hayo ameyasema leo Oktoba 21,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

“Matumizi holela ya dawa hasa za aina ya antibaiotiki huweza pia kuwaathiri binadamu kutokana na kula mabaki ya dawa hizo kwenye vyakula vinavyotokana na wanyama”almesema

Aidha, amesema hali hiyo ni tatizo kubwa linaloikabiri dunia kwa sasa na wafugaji wanapaswa kuzingatia ushauri unaotolewa ili kulidhibiti.

“Inakadiriwa kwamba kufikia 2030, watu zaidi ya milioni 10, watakufa kila mwaka kutokana na dawa kushidwa kuwatibu kwani vimelea vya magonjwa vitakuwa vimejenga usugu unaotokana na matumizi holela ya dawa kwa binadamu na mifugo”ameeleza

Dkt.Bitinyi amesema jumla ya sampuli 163,722 kutoka kwa wanyama mbalimbali zilipokelewa na kufanyiwa uchunguzi na utambuzi wa magonjwa.

Mtendaji Mkuu huyo amesema kuwa njia za uchunguzi zilizotumika ni pamoja na kuchunguza vimelea vya magonjwa kwa kutumia hadubini kuchunguza viaashiria vya uwepo wa kinga dhidi ya kimelea kwenye damu kwa kutumia ELISA na kipimo cha juu kabisa cha uchunguzi wa aina ya kimelea kwa kutumia vinasaba yaani PCR.

“Katika kipindi cha miaka mitano kati ya 2017/2018 hadi Septemba 30, 2022 jumla ya sampuli 163,722 kutoka kwa wanyama mbalimbali zilipokelewa na kufanyiwa uchunguzi na utambuzi wa magonjwa.

“Magonjwa muhimu yaliyotambuliwa kwa wingi ni mdondo/kideri, ndigana baridi, ndigana kali, ndui kwa kuku, homa ya nguruwe, kimeta, ugonjwa wa kutupa mimba, homa ya mapafu ya ng’ombe, homaya mapafu ya mbuzi, kichaa cha mbwa, sotoka ya mbuzi na kondoo”amesema Dk.Bitanyi

Kuhusu uzalishaji na usambazaji wa chanjo za mifugo, amesema Wakala inatekeleza jukumu hilo kupitia Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyoko Kibaha mkoani Pwani.

Amesema hivi sasa TVI, Kibaha inazalisha chanjo saba na uzalishaji kwa mwaka 2021/2022 ulifika dozi milioni 65.

“Kwakuwa chanjo haziwezi kuzalishwa na kusubiri wateja, kiwanda huzalisha kulingana na mahitaji ya soko. Uwezo kamili wa uzalishaji wa chanjo ni zaidi ya dozi milioni 100, kwa mwaka ambao hata hivyo bado haujafikiwa kutokana na uhitaji wa soko kuwa chini”amesama

No comments:

Post a Comment