NYAKANYENGE: DKT. SAMIA, WABUNGE NA MADIWANI WA CCM LAZIMA WASHINDE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 23, 2025

NYAKANYENGE: DKT. SAMIA, WABUNGE NA MADIWANI WA CCM LAZIMA WASHINDE

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wazazi CCM Taifa, Edwin Peter Nyakanyenge akinadi wagombea wa CCM ( Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ubunge - Patrobas Katambi na Madiwani wa CCM) wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini uliofanyika katika kata ya Chibe.

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Wakazi wa Chibe wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni
Wakazi wa Chibe wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni

Na Kadama Malunde – Shinyanga

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wazazi CCM Taifa, Edwin Peter Nyakanyenge amewataka wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa wagombea wote wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Nyakanyenge ametoa kauli hiyo Jumanne Septemba 23, 2025, wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM, Patrobas Katambi, uliofanyika katika kata ya Chibe.

“Sasa hivi kazi tuliyonayo ni moja tu, ni kutafuta kura za CCM. Tuhakikishe Dkt. Samia Suluhu Hassan anaongoza kura, Mbunge Katambi anaongoza kura na madiwani wote wa CCM wanaongoza kura. Tutembee kifua mbele kwa sababu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita yako dhahiri; sekta ya afya mnaona, shule mnaona, maji mnaona, umeme mnaona. Tutashindwaje kushinda? Tutashinda kwa kishindo,” amesema Nyakanyenge.

Aidha, amewataka wanachama wa CCM kuendelea na mikakati ya ndani kwa kushirikiana na makundi mbalimbali ya kijamii badala ya kutegemea mikutano ya hadhara pekee.

“Kila mmoja wetu ahakikishe anashawishi angalau kuanzia watu watano. Nimeshatoa maelekezo kwa Jumuiya ya Wazazi naomba na jumuiya nyingine zote zijipange kikamilifu. Tukifanya hivi mgombea wetu wa Urais Dkt. Samia lazima ashinde, wabunge lazima washinde na madiwani lazima washinde,” amesisitiza Nyakanyenge.
Awali kabla ya mkutano huo wa hadhara, Nyakanyenge amekutana na wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na kuwapa maelekezo ya kimkakati kuhusu kampeni na uchaguzi.

Kwa upande wake, Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, amewaomba wananchi kumpa kura nyingi yeye pamoja na wagombea wa CCM ili kuendeleza maendeleo yaliyofanikishwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, akisisitiza kuwa chama hicho ndicho chenye dira ya kweli ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi

“Mpango sahihi wa maendeleo ni CCM. Tumedhamiria kuendelea kuboresha maisha ya wananchi katika sekta zote ikiwemo elimu, afya na maji. Katika miaka mitano tumefanikisha miradi mikubwa, tunaomba kura zenu ili tuendelee kusonga mbele,” amesema Katambi.

Akieleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Katambi amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita amefanikisha miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi ndani ya Jimbo la Shinyanga Mjini, ikiwemo sekta za elimu, afya, maji na barabara.

Amebainisha kuwa bado kuna changamoto zinazohitaji kushughulikiwa, na akawaomba wananchi wampe ridhaa tena ya kuwa Mbunge wao ili aendelee kutatua changamoto hizo na kuwaletea maendeleo zaidi.

Naye Mgombea Udiwani Kata ya Chibe, Peter Kisandu, amewahimiza wananchi kuipigia kura CCM akisisitiza kuwa chama hicho kimejipanga kuimarisha huduma za afya, barabara na upatikanaji wa maji safi na salama katika kata hiyo na maeneo mengine ya manispaa.

ANGALIA PICHA
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wazazi CCM Taifa, Edwin Peter Nyakanyenge akinadi wagombea wa CCM ( Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ubunge - Patrobas Katambi na Madiwani wa CCM) wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini uliofanyika katika kata ya Chibe.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe, kulia ni Mgombea Udiwani Kata ya Chibe, Peter Kisandu
Mgombea Udiwani Kata ya Chibe, Peter Kisandu akinadi sera za CCM
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe akinadi sera za CCM
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wazazi CCM Taifa, Edwin Peter Nyakanyenge akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na kuwapa maelekezo ya kimkakati kuhusu kampeni na uchaguzi.

No comments:

Post a Comment