SAMIA KUPOKEA NA KUZINDUA RASMI CHUO CHA VETA KAGERA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 12, 2022

SAMIA KUPOKEA NA KUZINDUA RASMI CHUO CHA VETA KAGERA


Na WyEST,Kagera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania anatarajia kupokea na kuzindua Chuo kipya cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Kagera.

Halfa hiyo inatarajiwa kufanyika Jumatano tarehe 13 Oktoba, 2022. Katika Chuo hicho kipya kilichopo Burugo Nyakato Kagera.

Chuo hicho chenye karakana, vifaa na miundo mbinu ya kisasa kimejengwa kwa msaada wa Serikali ya China kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1,400 kwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika fani mbalimbali za ufundi na huduma.

Hayo yameelezwa na Prof. Adolf Mkenda Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipokagua maandilizi ya halfa hiyo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wa Nyakato, kagera na mikoa mingine kushiriki katika ufunguzi .

Ametumia nafasi hiyo kuelezea fursa mbalimbali za mafunzo zitokanazo na uwepo wa Chuo hicho na kuwataka vijana kujiunga na mafunzo ambayo yanalenga katika kujenga ujuzi.

No comments:

Post a Comment