![]() |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza na Wazee wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee Jijini Dodoma Oktoba 03, 2022. |
![]() |
Wazee wakiwa katika maandamano wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee yaliyofanyika Kitaifa Jijini Dodoma Oktoba 03, 2022. |
![]() |
Wazee wakiwa katika maandamano wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee yaliyofanyika Kitaifa Jijini Dodoma Oktoba 03, 2022. |
Na Okuly Julius-Dodoma
Vilevile Serikali iko katika mchakato wa kuanzisha miradi katika Makazi ya Wazee ili makazi hayo
yaweze kujiendesha na kupunguza utegemezi kwa Serikali.
Akizungumza leo Oktoba 3,2022 Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe George Simbachawene amesema kuwa Wadau wote nchini waunge mkono jitihada za Serikali kutokomeza vitendo vyote vya ukatili, kwa kuhakikisha kuwa kwa pamoja wanawezesha kutekelezwa kwa mikakati yenye lengo la kutokomeza Ukatili dhidi ya makundi yote ikiwemo Wazee,Wanawake na Watoto.
Mhe.Simbachawene amesema kuwa Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha masuala ya Wazee yanapewa kipaumbele na pale kunapotokea changamoto zinashughulikiwa. Moja ya maeneo
tunayoyapa kipaumbele ni huduma za Afya kwa Wazee Ili kuhakikisha hili, Serikali imeweza kuwatambua Wazee, kuwasajili na kuwapa vitambulisho vya msamaha wa matibabu na Bima za
Afya zilizoboreshwa.
Ambapo jumla ya Wazee 1,547,038 walitambuliwa katika Mikoa 26 kati yao Wazee 937,266 sawa na asilimia 60.6wamepatiwa Vitambulisho/Bima za Afya kwa ajili ya matibabu.
"Jambo hili ni la msingi sana kwani Mzee akiwa na afya njema inamuwezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo na za kijamii,"Amesema Simbachawene
Simbachawene ameongeza kuwa jumla ya Mabaraza 20,749 yameanzishwa nchini kote. Lengo la Mabaraza haya ni kuwapa fursa Wazee kukutana na kujadili mambo yao, lakini pia kutumika kama chombo cha ushauri katika jamii.
"Nimefurahi kusikia kwamba, miongoni mwetu leo mpo viongozi wa Mabaraza haya pamoja na wawakilishi wa Wazee toka Mikoa yote Nchini hii itasaidia kufikisha ujumbe huu kwa wazee,"Simbachawene
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima amesema serikali imeamua kutatua kero za wazee kupitia mabaraza yao.
Nae Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya humuma na maendeleo ya jamii Stanslaus Nyongo amesema bunge lipo tayari kujadili sera ya wazee ili itunguiwe sheria.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma una madirisha ya kuhudumia wazee katika vituo vya afya 357 huku zoezi la kuwapatia vitambulisho likiendelea.
Akizungumza katika Maadhimisho hayo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amebainisha kuwa, TAMISEMI imeendelea na zoezi la kuwatambua wazee na hadi sasa imetambua 2117637 kutoka Mikoa yote 26 bapo wanaume ni 1382468 na wanawake 735169.
"Tumetoa Bima ya Afya ya Jamii kwa Wazee ili wapate huduma kwenye vituo vya Afya ngazi ya msingi kuanzia zahanati Hadi hospitali za Wilaya" amesema Dkt. Grace.
Dkt. Grace ameongeza kuwa, katika kukabiliana na changamoto ya Maafisa Ustawi wa Jamii, kibali limetolewa cha kuajiri Maafisa hao 65 ambao wamepangwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wakatekeleze sera ya Mzee kwanza.
Akizungumza kwa niaba ya wazee wote hapa nchini Mwenyekiti wa Baraza la Wazee taifa Mzee Lameck Sendo ameiomba serikali kuchukua hatua kali za kisheria katika kuwalinda dhidi ya ukatili na unyanyasaji wanaofanyiwa ndani ya jamii ili mchango wao katika taifa uzidi kuthaminiwa.
Katika maadhimisho hayo Wazee wamewakilishwa na Wazee 3000 kutoka maeneo mbalimbali nchi nzima katika siku hii iliyokuwa inabebwa na kauli mbiu isemayo "Ustahimilivu na mchango wa Wazee ni muhimu kwa Maendeleo ya Taifa”
No comments:
Post a Comment