MRADI WA MWANAMKE JASIRI KUWAFIKIA WANAWAKE 4000 DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 3, 2022

MRADI WA MWANAMKE JASIRI KUWAFIKIA WANAWAKE 4000 DODOMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Newface Creation Alex Kapandila akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 2,2022 Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Mwanamke Jasiri ambao utawafikia wanawake 4000.
Mwenyekiti wa Tasisi ya Newface Creation Abdul Jimson a akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 2,2022 Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Mwanamke Jasiri ambao utawafikia wanawake 4000.

NA FRED ALFRED DODOMA

TAASISI ya Newface Creation imesema inatarajia kuwawezesha kiuchumi vijana wa kike 4000 waishio vijijini kupitia wa mradi mwanamke jasiri.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini hapa,Mwenyekiti wa Tasisi ya Newface Creation Abdul Jimson amesema mradi huo utaanzia katika wilaya ya Chamwino kwa kugawa taulo za kike na kutoa misaada kwa wazee wasio jiweza.

“Kwa Mkoa wa Dodoma tunatarajia kuwafikia vijana wasiopungua 4000 na tutaanzia wilaya ya Chamwino na Kongwa ambapo tutaweza kuwakimu mahitaji yao wanawake wenye uhitaji,”alisema

Ameongeza kuwa: “Lengo la kuelekeza mradi huu katika maeneo ya vijijini ni kutokana na kuonekana kuwa na changamoto nyingi zaidi kuliko mjini pia hawapewi kipaumbele wanaishi kama wakoloni.Tumewahi kufanya miradi mingine ikiwemo ugawaji wa madaftari kwa watoto yatima,mkuranga,Bagamoyo na Tuwangoma na kwa sasa tunarudisha nguvu kubwa Dodoma katika wilaya ya chamwino.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Newface Creation Alex Kapandila amewakaribisha wadau kuwasaidia ili waweze kutatua changamoto za watanzania wengi ambao wanahitaji msaada.

Ameiomba serikali kuendelea kushirikiana na tasisi mbalimbali za kiraia katika kufikisha msaada kwa jamii.

“Unahitajika msaada kutoka kwa watu wakubwa ili tuweze kuwafikia wahitaji wengi na ukiangalia uhalisia nchini yetu ni kubwa na serikali haiwezi kuwafikia watu wote hivyo mashirika yanachukua nafasi hiyo,”alisema

Naye Katibu Tawala wa Newface Creation Barika Mwaisaka amesema katika kumuunga mkono Rais Samia kwani amekuwa akipambana katikakuhakikisha ndoto za wanachi zinafikiwa.

Amesema kupitia mradi wa mwanamke jasiri tunaahidi kufanikisha ndoto za wanawake wengi za kujikwamua kiuchumi.

No comments:

Post a Comment