Na Okuly Julius-Dodoma
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff mbele ya waandishi wa habari leo Oktoba 3,2022 Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za wakala huyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
"Hadi sasa tumejenga madaraja 110 yenye thamani ya Shilingi bilioni 5 ambapo gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia 50. Madaraja hayo yamejengwa katika mikoa ya Kigoma 72, Singida 13, Tabora 3, Kilimanjaro 6, Mbeya 2, Arusha 4, Mrorgoro 2 na Iringa 9,"Amebainisha Seff
Mhandisi Victor amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Wakala hiyo na kuanza majukumu yake mnamo Julai 1,2017 na kukamilika tarehe 30 June 2021 jumla ya Shilingi 1,297.79 milioni fedha za ndani zilitumika.
Ambapo Katika kipindi hicho jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 24,979.24 zilifanyiwa matengenezo, kilometa 955.35 zilijengwa kwa kiwango cha lami na kilometa 16,857.82 zilijengwa/karabatiwa kwa kiwango cha changarawe. Aidha, jumla ya madaraja 231 (kutoka Madaraja 2,960 hadi 3,191) na Makalvati 1,325 yamejengwa (kutoka Makalvati 67,992 hadi 69,317)
Katika kipindi hicho jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 24,979.24 zilifanyiwa matengenezo, kilometa 955.35 zilijengwa kwa kiwango cha lami na kilometa 16,857.82 zilijengwa/karabatiwa kwa kiwango cha changarawe.
Ambapo jumla ya madaraja 231 (kutoka Madaraja 2,960 hadi 3,191) na Makalvati 1,325 yamejengwa (kutoka Makalvati 67,992 hadi 69,317).
Akizungumzia kuhusu mpango mkakati wa pili wa TARURA wa 2021 mpaka 2026 umepanga Kuondoa vikwazo kwenye mtandao wa barabara za Wilaya ili ziweze kupitika misimu yote,Kupandisha hadhi (upgrading) barabara za udongo kuwa za Changarawe/Lami kwa kuzingatia vipaumbele vya kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa magari katika majiji, manispaa na miji.
Mhandisi Victor Seff ameongeza kuwa kuanzia mwaka 2021/22 hadi 2026/27 lengo la TARURA ni kuwa mtandao wa barabara za lami utaongezeka kwa km 1,450.75 (kilometa 2,404.90 - 3,855.65), changarawe km 73,241.57 (kilometa 29,116.57 - 102,358.14) na madaraja 3,808 (toka 2,812 hadi 6,620) ambapo fedha zitakazotumika kwenye mpango huu zinakadiriwa kuwa Zaidi ya Shilingi trilioni 4.2.
"Lengo la Mpango Mkakati wetu wa pili ni kuwa ifikapo 2025/26 asilimia 85 ya mtandao wa barabara za Wilaya chini ya TARURA zitakuwa zinapitika kwa misimu yote na nyakati za mvua hapatakuwa na taharuki inayojitokeza sasa kwa maeneo mengi kutofikika,"Amesema Mhandisi Victor Seff
Aidha,Mhandisi seff amesema kwa Mwaka wa fedha 2022/23 ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa pili ambapo TARURA imetengewa bajeti ya jumla ya Shilingi bilioni 838.16 ambapo kati ya hizo Shilingi bilioni 776.63 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 61.53 ni fedha za nje.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amesema serikali inaaendelea kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha inapeleka fedha za kutosha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya barabara hapa nchini.
"Nia ya serikali ni kuifanya nchi ifunguke na kufikika kila eneo na hilo linawezekana hata ukiangalia bajeti zinazelekezwa huko TARURA ni nzuri sana hivyo itawasaidia katika kukamilisha mipango yao na naamini kwa mikakati hii hakuna haja ya kuwa na wasiwasi nchi itafikika na itasaidia kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi kwa ujumla,"Amesema Msigwa
Lengo la kuanzishwa TARURA limezingatia ukweli kuwa takribani asilimia 70 ya watanzania wanaishi vijijini na mojawapo ya changamoto ya maendeleo inayowakabili watanzania hao ni kutokuwa na barabara za vijijini za uhakika za kuwawezesha kutoa mazao shambani na kuingiza pembejeo za kilimo kwa ajili ya shughuli za ki uchumi lakini pia kuwawezesha kufikia huduma muhimu za jamii kama Hospital, Shule, Masoko, nk.
Hivyo Serikali iliamua kuanzisha TARURA ili kukabiliana na mabadiliko katika sekta ya Barabara kwa nia ya kuboresha huduma na kuongeza ufanisi katika kusimamia menejimenti ya barabara za Wilaya ambazo zina mchango mkubwa kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii vijijini lakini pia kukabiliana na changamoto zilizojitokeza wakati jukumu la Menejimenti ya Mtandao wa Barabara za Wilaya lilipokuwa chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) 184.
No comments:
Post a Comment